Instagram imekuwa ikifanya mabadiliko ya App zake kila siku, Hivi karibuni moja ya mabadiliko ni pamoja na uwezo mpya wa kupost picha au video zaidi ya moja kwa wakati mmoja kupitia sehemu ya Stories. Hapo awali ilikuwa ni lazima kupost picha au video moja kwenye stories baada ya kumalizika kisha ndipo uweze kupost picha au video nyingine kupitia sehemu hiyo.
Lakini sasa utakuwa na uwezo wa kupost picha au video zaidi ya moja kupitia sehemu mpya ambayo inatokea pale utakapo fungua sehemu ya Stories, sehemu hiyo inapatikana juu upande wa kulia na utaitumia pale tu utakapokuwa unataka kupost Stories zaidi ya moja.
Sehemu hiyo imeandikwa (Select Multiple) na inafanya kazi sawa sawa na sehemu ile ya kupost picha na video za kawaida ambapo pia unaweza kuchagua picha au video nyingi kwa wakati mmoja. Sehemu hiyo mpya kwenye Stories itakuwezesha kuchagua picha au Video za stories zisizozidi 10.
Kwa sasa tayari sehemu hii ipo kwenye toleo jipya la programu ya Instagram ya mfumo wa Android, hivyo kama bado hujapata sehemu hii basi hakikisha una update programu yako ya Instagram na utaweza kuona sehemu hii pale utakapo fungua sehemu ya Stories. Kwa watumiaji wa iOS sehemu hii itawafikia siku za karibuni.