Kama wewe ni mtumiaji wa App ya Instagram lazima utakuwa umeona mabadiliko machache ambayo yamefanyika kwenye app hiyo. Kama bado hujaona mabadiliko hayo basi kwenye makala hii nitaenda kukujuza angalau mabadiliko machache ambayo tayari yapo kwenye akaunti yetu ya Instagram ya Tanzania tech.
TABLE OF CONTENTS
Aina Mpya ya Profile
Kwa kuanza tuanze na aina mpya ya profile, kama umetufuata kwenye akaunti yetu ya instagram basi hili litakuwa sio geni kwako kwani hivi karibuni instagram inatarajia kufanya mabadiliko ya profile ambayo yatawezesha app hiyo kuangalia zaidi akaunti ya mtu na sio idadi ya follower.
Kwenye profile hiyo mpya idadi ya follower na follow itakuwa haionekani kama hapo awali, kadri unavyozidi kuwa na follower wengi zaidi ndipo sehemu hiyo inavyokuwa haionekani zaidi. Hapo chini utaona jinsi profile ilivyokuwa hapo zamani na itakavyokuwa siku za karibuni.
Profile ya Zamani
Nadhani unaweza kuona tofauti iliyopo, kwani kwenye profile ya zamani unaweza kuona sehemu ya idadi ya follower, following pamoja na idadi ya post ikiwa inaonekana zaidi kuliko kwenye profile ya sasa.
Profile ya Sasa
Kama unavyoweza kuona sehemu ya idadi ya follower na following haionekani zaidi kama ilivyo mwanzo, kwa sasa jina ndio linalo onekana zaidi, pamoja na sehemu ya wasifu au Bio. Pia unaweza kuona idadi ya post haipo kabisa kwenye profile ya sasa.
Kwa sasa kuna sehemu mpya ua kushare pamoja na sehemu mpya ya ku-copy link, sehemu hizi zipo sehemu tofauti na zilipokwepo awali. Kwa sasa instagram imeweka sehemu hizi kwenye kitufe kimoja ambacho ndio kina mambo yote haya.
Sehemu za Kucopy link na Kushare Zamani
Kama unavyoweza kuona zamani ili kushare picha ya mtu au ku-copy link ya post ni lazima kubofya sehemu ya vidoti vitatu iliyopo juu upande wa kushoto kwenye post husika, lakini sasa sehemu hizi zimebadilishwa.
Sehemu za Ku-copy link na Kushare Sasa
Kama unavyoweza kuona sasa sehemu iliyopo pembeni ya kitufe cha comment ndio yenye sehemu hizi za ku-copy, share pamoja na sehemu mpya za Reply pamoja na Add to Story.
Sehemu mpya za Reply na Add to Story
Sehemu nyingine zote zinafanya kazi kama kawaida lakini pia kuna sehemu mpya ambazo zimeongezwa kwenye kitufe cha share, sehemu hizo ni Add to Story na Sehemu ya Reply. Sehemu ya Reply yenyewe inakusaidia kujibu meseji au kumtumia mtu meseji ambayo inakuja na picha ya post husika.
Sehemu ya Add to Story yenyewe inakupa nafasi ya kuweka picha ya mtu kwenye sehemu yako ya Story moja kwa moja, unapo bofya sehemu hiyo post hiyo inaenda kwenye sehemu yako ya Stories moja kwa moja ikiwa pamoja na username ya mtu mwenye picha.
Sehemu hizi zote bado hazijapatikana kwa baadhi ya watu hivyo unaweza kusione sehemu hizo na pia kwa baadhi ya profile unaweza kuona sehemu hizi. Kwa sasa kama unataka update za mara kwa mara kuhusu sehemu mpya za kwenye mtandao wa instagram hakikisha una-fuata ukurasa wetu wa Instagram hapa.