Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Kuboreshwa Kwa Ajili ya Watu Wasioona Vizuri

Ni wakati sasa wote tufurahie matumizi ya Internet kwa pamoja
instagram kwa wasioona vizuri instagram kwa wasioona vizuri

Pamoja na changamoto inayowapata watu wasiona wakati wa kutumia internet, kwenye nchi mbalimbali bado jitihada zinaendelea kuwezesha kuleta usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwa pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii. Katika kuendeleza jitihada hizo, hivi karibuni mtandao wa Instagram unakuja na sehemu mpya mbili ambazo zitakuwa zinawasaidia zaidi watu wasioona kuweza kutumia mtandao huo kwa urahisi zaidi.

Sehemu hizi mpya zitamuwezesha mtu yoyote anayeweka picha kwenye mtandao huo kuweza kuandika maneno kwenye sehemu maalum maneno ambayo yatakua yanaelezea kuhusu picha hiyo anayo weka inaonyesha nini.

Advertisement

Tofauti na sehemu ya kawaida ya description sehemu hii mpya itakuwa inauwezo wa kufanya kazi sambamba na sehemu ya speech inayopatikana kwenye smartphone nyingi za siku hizi. Sasa kama mtu huyo atakuwa amewasha sehemu hiyo, Kupitia instagram mtu mwenye matatizo ya kutoona vizuri ataweza kusikiliza kile kilicho andika na hivyo kuweza kujua kuhusu picha hiyo inaonyesha nini.

Kwa mujibu wa Instagram, sehemu hiyo itakuwa inapatikana wakati unaweka picha na utakuwa na uwezao wa kutachagua advanced settings na kisha kuchagua sehemu ya Write Alt Text na hapo utaweza kuweka maelezo yanayo elezea picha yako kwa maneno kwaajili ya watu wasioona vizuri.

Sehemu nyingine ambayo itakuwa inasaidiana na hiyo ni sehemu ya Automatic, sehemu hii itakuwa inatumia teknolojia ya kisasa kuweza kuangalia picha na kuweza kuelezea kwa mtu asiyeona vizuri hata kama hakuweka maneno yanayo elezea picha hiyo wakati wa kupost. Sehemu hizi zote mbili zinategemewa kuja hivi karibuni kupitia app zote za Instagram za iOS pamoja na Android.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use