Hivi karibuni kumezuka gumzo ambapo imethibitishwa kuwa instagram sasa ita-anza kutuma meseji maalumu pale tu mtu atakapo chukua screenshot ya picha au meseji ambazo zipo kwenye private meseji.
Katika picha hapo chini ni moja kati ya meseji hiyo inavyoonyesha pale mtu atakapo chukua screenshot ya picha au meseji za mtu. Sehemu hiyo mpya ambayo haijajulikana kama imeshanza kuonekana kwa watu wote imechukuliwa kwa namna tofauti ikiwa wapo walio furahia na walio chukia ujio wa sehemu hiyo.
Instagram imeamua kufuata nyayo za mtandao wa snapchat ambayo nayo pia hutuma meseji maalum pale mtu atakapo chukua screenshot ya picha ama meseji za mtu pale ambapo haitakiwi kufanya hivyo.
Je nini maoni yako kuhusu sehemu hiyo mpya.? tuandikie hapo chini au pia unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.