Mtandao wa instagram kupitia programu zake za instagram za Android na iOS, leo imetangaza sehemu mpya ambayo itakuwezesha kuhifadhi picha za mtu yoyote kwenye sehemu maalum au (private collection).
Kuanzia leo watumiaji wa mtandao huo wataanza kuona sehemu yenye mshale maarufu kama, bookmark icon ambapo kwa kubofya hapo utaweza kuhifadhi picha yako au ya mtu yoyote kwenye sehemu maalum.
Sehemu hii inakuja kwenye toleo jipya la mtandao wa instagram wenye toleo la Instagram version 10.2. Unaweza kuangalia update za programu hiyo sasa ili kupata sehemu hiyo mpya kwenye programu hiyo maarufu ya kijamii.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.