Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Itaruhusu Watumiaji Kupakua Data za Matumizi

Bado haija julikana matumizi rasmi ya sehemu hiyo yatakuwa yapi
Instagram Download Data Instagram Download Data

Hivi karibuni msemaji wa mtandao wa Instagram kupitia tovuti maarufu ya Techcrunch alisema kwenye maojiano kuwa, instagram inategemea kuleta sehemu mpya maalum ambayo itakuwezesha wewe kupakua (download) data zako za matumizi ya mtandao wa Instagram.

Kupitia msemaji huyo, bado haijajulikana matumizi halisi ya sehemu hiyo yatakuwa yapi au sehemu hiyo itafanya kazi kwa namna gani, kati ya kumuwezesha mtumiaji ku-hifadhi data zake kwaajili ya matumizi ya baadae (backup) kama ilivyo sehemu ya backup kwenye WhatsApp, au kupakua data hizo kwaajili ya kuona matumizi yako halisi kwenye mtandao wa Instagram kama ilivyo kwenye mtandao wa Facebook.

Advertisement

Kwa sasa sehemu ya kupakua data za matumizi yako inapatikana kwenye mtandao wa Facebook ambapo unaweza kutumia sehemu hiyo kuweza kujua matumizi yako ya mtandao wa Facebook ikiwa pamoja na kurasa ulizopitia pamoja na vitu ulivyo tafuta kwa kutumia sehemu ya kutafuta kupitia mtandao huo.

Kwa sasa unaweza kupakua data zako za matumizi ya mtandao wa facebook kwa kuingia kwenye akaunti yako kwa kutumia kompyuta au kama unatumia simu hakikisha unatumia browser au kisakuzi. Kisha baada ya kuingia kwenye ukurasa wako wa Facebook, bofya Settings inayo patikana upande wa kulia juu, kisha bofya Download a copy of your Facebook data, sehemu inayopatikana chini ya sehemu ya General Account Settings.

Kwa watumiaji wa simu za mkononi sehemu hii haipo kwenye programu za Facebook za Android au iOS hivyo itakubidi kuingia kwenye uwanja huo wa Facebook kwa kutumia kompyuta au kwa kutumia kisakuzi au browser ya simu yako, mfano Google Chrome.

Hata hivyo bado haijajulikana ni lini sehemu hiyo itakuja kwenye mtandao wa instagram na tofauti na mtandao wa Facebook tunatumaini sehemu hii itakuwepo kwenye programu za Instagram za iOS na Android kwani matumizi halisi ya mtandao huo yanafanyika zaidi kwenye programu hizo kuliko kwenye tovuti ya mtandao huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use