Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Kuleta Link Maalum Kwenye Sehemu ya Instagram Stories

Instagram yaongeza sehemu mpya za mentions na links kwenye sehemu ya Instagram Stories
Instagram stories Instagram stories

Ni miezi mitatu imepita toka Instagram ilipotangaza sehemu mpya maarufu kama instagram stories, sehemu hiyo ambayo ina fanana sana na ile ya kwenye mtandao wa snapchat imefanya watu kutumia programu ya Instagram kwa namna mpya lakini sio ya kipekee, hii ni kutokana na sehemu hiyo kufanana sana na ile ya programu ya snapchat. Pengine hii ndio sababu ya Instagram kuamua kuongeza sehemu mpya kwenye sehemu hiyo ya stories ili kutofautisha sehemu hiyo na ile ya kwenye mtandao wa snapchat.

Toleo hilo Jipya la programu ya Instagram linategemewa kuja na sehemu mpya za mentions pamoja na links kwenye instagram stories, jinsi sehemu hizo zinavyofanya kazi hapa watumiaji wataweza kuweka link kwenye “stories” chini kidogo ya picha za sehemu hiyo ambapo kutakua na kitufe chenye maandishi “see more” ambayo ukibofya hapo utapelekwa kwenye tovuti kwa kutumia browser ya mtandao huo wa instagram. Sehemu hiyo ya link kwenye stories itakuwa pekee kwenye akaunti zilizo hakikiwa (Verified)

Advertisement

link

Kuhusu sehemu mpya ya Mention hapa watumiaji wataweza kuandika jina la mtu kwenye stories kwa kuanza na alama ya “@” ikifatiwa na jina la mtu unaetaka kumuunganisha kwenye stories zako. baada ya kuweka jina la mtu kwenye sehemu hiyo jina hilo litaonekana likiwa limepigiwa mstari ndani ya picha kwenye sehemu hiyo ya stories.

mention

Hata hivyo Instagram imeamua kuongeza sehemu hizo kutokana na watu mbalimbali na makampuni kutumia sehemu hiyo ya stories kutangaza biashara zao. sehemu hizo zinategemewa kuja hivi karibuni hivyo ni vizuri ukiona update za programu hiyo hakikisha unadownload ili kujaribu sehemu hizo.

Je unasemaje kuhusu sehemu hii mpya.? tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use