Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Kuja na Rooms Kupitia Sehemu ya Instagram DM

Sasa utaweza kufanya mikutano na marafiki kupitia instagram DM
Instagram Kuja na Rooms Kupitia Sehemu ya Instagram DM Instagram Kuja na Rooms Kupitia Sehemu ya Instagram DM

Hivi karibuni kampuni ya Facebook ilitangaza ujio wa sehemu mpya ya Rooms kupitia kwenye programu yake ya Facebook Messenger. Kama haitoshi hivi karibuni habari mpya zinasema kuwa WhatsApp pia inategemewa kupata sehemu mpya ya Rooms ambayo itawazesha watumiaji kufanya mikutano kwa njia ya video kupitia mtandao wa WhatsApp bila hata kuwa programu hiyo.

Instagram Kuja na Rooms Kupitia Sehemu ya Instagram DM

Advertisement

Sasa mbali na WhatsApp, hivi karibuni instagram inategemea kuleta sehemu ya Rooms kupitia sehemu Direct Messenger. Sehemu hii itakuwa inapatikana ndani ya Instagram kwa kubofya sehemu ya DM iliyopo juu upande wa kulia kisha bofya sehemu ya kitufe cha video na moja kwa moja utaweza kuona sehemu ya kutengeneza Rooms ambayo itakua juu kabisa.

Instagram Kuja na Rooms Kupitia Sehemu ya Instagram DM

Kwa sasa unaweza kutumia sehemu ya Rooms kupitia Facebook Messenger, na utaweza kufanya mikutano na watu wako wa karibu kwa njia ya video kwa haraka kabisa. Unaweza kutumia sehemu ya Rooms kwenye programu ya WhatsApp na Instagram DM hivi karibuni.

Hakikisha una update application yako ya Instagram kupitia soko la Play Store au App Store kisha angalia sehemu ya DM na moja kwa moja utaweza kuona sehemu hiyo au kama bado hujaona sehemu hiyo basi unaweza kuendelea kusubiri ndani ya siku chache na utaweza kuona sehemu hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use