Hivi karibuni mtandao wa Instagram umeonekana kufanya majaribio ya sehemu mpya kabisa ya Nametags, sehemu hii ni kama ile inayopatikana kwenye programu ya Snapchat inayojulikana kama Snapcode, ambapo mtu ataweza kutengeneza QR Codes maalum ambazo utaweza kuzitumia kupata ukurasa au kushiriki ukurasa wako wa instagram kwa urahisi zaidi.
Sehemu hiyo mpya itaweza kufungua sehemu ya Stories kwa haraka na kwa kuscan Nametags ya mtu utaweza kufuata akaunti ya mtu moja kwa moja na pia utaweza kushiriki stories au profile yake na watu wengine kwa haraka zaidi.
Ujio wa sehemu hii utakuja sambamba na sehemu nyingine mpya ndani ya kamera ya Stories ambayo itakusaidia kutengeneza Nametags kwa kuchagua vitu mbalimbali kama picha, emoji pamoja na picha maalum zenye sura au picha ya mwenye akaunti katikati.
Kwa sasa bado sehemu hii haijatoka rasmi na bado haijajulikana lini sehemu hii itakuja rasmi kwenye programu za instagram. Hivi leo Instagram kupitia msemaji wake imeongea na mtandao wa Techcruch na kuthibitisha kuwa ni kweli inafanya majaribio ya sehemu hiyo. Kwa habari zaidi kuhusu ujio wa sehemu hii endelea kutembelea Tanzania Tech.