Kwa sasa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram watu wote wana uwezo wa kufuata (follow) mtu au akaunti flani, lakini hivi karibuni imeripotiwa kuwa Instagram inafanya majaribio ya mtu kuwa na uwezo wa kufuata (follow) hashtag.
Mtandao wa kijamii wa #Instagram unafanyia majaribio ya kuleta uwezo mpya wa kuweza kufuata (follow) hashtag. Soma zaidi hapa > https://t.co/a9fGQwsYNq pic.twitter.com/W5DOv52vh5
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) November 11, 2017
Sehemu hiyo ambayo imesemekana kuja kuwa ya muhimu sana, inategemewa kukupa uwezo wa tofauti kwani utakuwa huna haja ya kufuata (follow) akaunti flani ili kupata picha na habari mpya za mtu au biashara hiyo, bali sasa utaweza kufuata (follow) hashtag ambayo akaunti hiyo inatumia mara kwa mara na utapata taarifa pindi akaunti au mtu huyo atakapo itumia hashtag hiyo.
Hata hivyo Instagram kwa sasa inafanya majaribio ya sehemu hiyo kwa watu wa chache na bado haijajulikana kuwa ni lini sehemu hiyo itatolewa kwa watumiaji wote wa mtandao huo, Instagram imekuwa ikifanya majaribio ya sehemu mpya mbalimbali huku baadhi ya sehemu hizo zikiwa bado hazikufanikiwa kutangazwa rasmi mpaka leo.
Kwa sasa inabidi tuendelee kusubiri ili kujua zaidi kuhusu sehemu hiyo, je wewe unaonaje tuambie nini maoni yako kuhusu sehemu hii..? unahisi itakuwa msaada au ndio itasababisha followers wako kupungua au kutoku ongezeka sababu sasa wana wanafuata (follow) hashtag, na sio akaunti yako.? tuambie kwenye maoni hapo chini.
Unaweza kuendelea kutembelea Tanzania tech kila siku au kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store ili kupata taarifa zaidi za sehemu hiyo pindi tu itakapo tangazwa rasmi.