Instagram hivi karibuni imefanya mabadiliko kadhaa kwenye sehemu ya IGTV, kama ufahamu kuhusu IGTV hii ni sehemu mpya ambayo ilizinduliwa na instagram mwaka 2018 na uruhusu watumiaji wa mtandao huo kuweka video zenye mda zaidi ya dakika moja.
Awali sehemu hii ilikuwa ikiruhusu kuweka video za wima pekee na ambazo kwenye simu zingeweza kuonekana kwa ukaribu zaidi na kwa urahisi. Lakini hivi karibuni instagram imefanya mabadiliko ya sehemu hiyo na sasa unaweza kuweka hata video za mlalo (usawa) ambazo mara nyingi hizi hutumika kwenye mitandao kama Youtube na Facebook.
Kwa mujibu wa ripoti kupitia blog ya mtandao wa instagram, sehemu hii tayari imesha wezeshwa kwa watumiaji wote na utaweza kuweka video zako za usawa moja kwa moja kwenye channel yako ya IGTV.
Kwa sasa kama unataka kuangalia video yoyote ya IGTV kwa usawa, unatakiwa kubofya kitufe cha pembe nne kinacho onekana upande wa kulia juu na moja kwa moja video unayo angalia itakuwa kwa mfumo wa usawa. Vilevile kama unataka kurudisha video iwe wenye mfumo wa wima unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe cha pembe nne kinacho onekana chini upande wa kulia.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech, pia usisahau ku-subscribe kwenye channel yetu ili kujifunza maujanja mbalimbali kwa vitendo.