Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii ni muhimu sana kuwa na uwezo wa kupakua picha au video kwa urahisi. Japokuwa kuna apps nyingi sana zinazoweza kusaidia kupakua video na picha kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini sio kila wakati app hizi hufanyakazi.
Kuliona hili leo nimekueletea njia fupi na rahisi ambayo unaweza kutumia kupakua video au picha ya aina yoyote kutoka kwenye mtandao wa Instagram.
Njia hii ni bora sana kuliko njia ya kutumia app kwani utaweza kupakua video kwa haraka na bila kupoteza muda mwingi kuinstall app, au kuangalia matangazo kwanza ndio uruhusiwe kupakua video au picha.
Kwa kuanza moja kwa moja tembelea link hapo chini, kisha paste link yoyote baada ya kucopy kwenye app ya Instagram.
Baada ya hapo paste link hiyo kwenye sehemu iliyo andikwa “Paste URL Instagram” au unaweza kubofya sehemu ya “Paste”. Baada ya hapo bofya kitufe cha “Download”.
Baada ya hapo moja kwa moja bofya kitufe cha kupakua video na utaweza kupakua video au picha mara moja bila kuhitaji app app ya aina yoyote. Njia hii inafanya kazi kwa watumiaji wa simu za aina zote “Android na iOS” na pia hata kwenye kompyuta za aina zote “Windows na MacOS”.
Bila shaka utaweza kutumia njia hii mara kwa mara kwani binafsi njia hii imekuwa bora kuliko kutumia apps kwenye simu yangu.
Kama unataka kujifunza maujanja zaidi hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech, kupitia play store. Pia kama unataka kupata makala hizi za Kiswahili, bofya sehemu ya Menu > Swahili Site kisha funga na fungua app kusoma tovuti ya Kiswahili.