Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Kuja na “Close Friends” Njia Mpya ya Kushare Stories

Sasa shiriki picha zako na watu wako wa karibu kupitia Instagram
Instagram Close Friend Instagram Close Friend

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Instagram ni lazima hadi sasa umeweza kuona sehemu mpya ya Close Friend, sehemu hii ilitangazwa kufanyiwa majaribio rasmi mapema june mwaka 2017 na kipindi hicho sehemu hiyo ilikuwa ikiitwa Favorite.

Kwa kipindi hicho Favorite ilikuwa ni sehemu ambayo inaruhusu mtumiaji wa Instagram kuweza kutumia mtandao huo kwa karibu zaidi na watu ambao anawajua kuliko watu usio wajua. Kama unavyojua kupitia mtandao wa Instagram sasa, unaweza kuona hata profile za watu ambao hata huwajui kwa namna yoyote.

Advertisement

Sasa sehemu hii mpya ya Close Friend, inaruhusu kuweza kushiriki picha zako na marafiki unao wajua zaidi kuliko ambao huwajui. Sehemu hiyo itakuwa inafanya kazi kupitia sehemu ya Stories na ili kuweza kutumia sehemu hiyo, unatakiwa kufungua Menu mpya iliyoko kwenye profile yako juu upande wa kulia, kisha chagua sehemu ya Close Friend. Baada ya hapo chagua Suggestion kisha utaona list ya marafiki ambao instagram inadhani uko nao karibu, tafuta marafiki unaowajua kisha bofya sehemu ya Add mbele ya jina la mtu huyo.

Instagram Kuja na "Close Friends" Njia Mpya ya Kushare Stories

Baada ya kuweka marafikizako kwenye list ya Close Friend, basi utakuwa na uwezo wa kushare nao picha zako za Stories kwa urahisi zaidi. Ili kuweza kushare storie yako na watu wako wa karibu au Close Friend, ingia kwenye sehemu ya kupost stories inayopatikana kwenye kitufe cha kamera kilichopo juu upande wa kulia, chagua picha au piga picha mpya kisha wakati unataka kupost angalia upande wa kushoto chini utaona sehemu imeandikwa Close Friend, bofya hapo na utaweza kushare stories yako moja kwa moja na watu wako wa karibu.

Sehemu hii tayari inapatikana kwenye app za Instagram za Android pamoja na iOS na unaweza kutumia sehemu hiyo sasa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use