Kama akaunti yako ya instagram ilishawahi kudukuliwa ni wazi unajua jinsi livyo ngumu kurudisha akaunti yako. Mbali na ugumu uliopo pia unaweza kutoa pesa nyingi sana hasa hapa Tanzania kwa watu ambao wana uwezo wa kurudisha akaunti yako.
Kuliona hili hivi karibuni Instagram imeanza kufanya majaribio ya sehemu mpya ambayo itaweza kusaidia kurudisha akaunti yako ya Instagram pale inapo dukuliwa (Hacked). Kwa mujibu wa tovuti ya Vice, Instagram imeanza kufanya majaribio ya sehemu hiyo ambayo ikuwa inatumia barua pepe na namba ya simu kuweza kurudisha akaunti ya mtu iliyodukuliwa.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, watu wengi hudukuliwa akaunti zao za instagram kwa kubofya kwenye barua pepe inayotumwa na mdukuaji inayo fanana na barua pepe kutoka Instagram, barua pepe inayokutaka kubadilisha password huku ikidai kuwa kuna mtu alikuwa akitaka kudukua akaunti yako. Hata hivyo pale unapo bofya kwenye barua pepe hiyo na kuweka password zako ndio hapo mdukuaji huweza kupata password zako na kudukua akaunti yako.
Sasa kupitia sehemu hiyo mpya, Instagram itakuwa inatuma barua pepe au meseji yenye tarakimu sita ambazo zitasaidia kurudisha akaunti yako, hata hivyo kama mdukuaji amedukua barua pepe yako basi instagram itahakikisha mtu atoweza kutumia tarakimu hizo kama hatumii kifaa ambacho kilitumika kutengeneza akaunti usika.
Mbali na hayo pia kwa mujibu wa tovuti hiyo, njia hiyo hiyo pia itatumika kulinda username ya mtu pale mdukuaji atakapo badilisha username kwa ajili ya kutumia kwenye akaunti nyingine.
Kwa sasa bado sehemu hii ipo kwenye majaribio na bado hakuna taarifa zaidi za namna sehemu hii itakavyokuwa inafanya kazi. Kwa taarifa zaidi kuhusu sehemu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kama unataka kujua njia za kuzuia akaunti yako kudukuliwa unaweza kusoma hapa.