Nilishaandika kuhusu sifa za simu mpya ya Infinix ZERO X na hii ni baada ya kuzinduliwa mubashara kupitia tafrija iliyo andaliwa na wataalamu wa Anga wanao jihusisha maswala ya nyota na mwezi ‘Royal Observatory Greenwich’.
Baadhi ya waandishi tulipata nafasi ya kushiriki semina ya Infinix ZERO X dhumuni ikiwa ni kujifunza zaidi namna kila sifa ya simu hiyo ilivyo na faida katika maisha yetu ya kila siku.
Kwanza kabisa sifa kuu ya Infinix ZERO X ni kamera na Infinix imewekeza zaidi kwenye kamera nyuma ikiwa na kamera tatu na kamera kuu ni MP 108 na nyuzi 60X periscope za kuzoom kifaa kwa ukaribu zaidi kabla ya kupiga picha.
60X periscope imethibitika kuwa na uwezo wa kupiga picha za Anga na hii ni baada wataalamu wa nyota kufanya jaribio hilo kama inavyo onekana kwenye picha hiyo.
Nikiwa kama mjuzi wa maswala ya tech ni Dhahiri kampuni ya simu inahitaji pongezi series ya ZERO safari hii imekuja na mapinduzi kubwa. Infinix ZERO X ni simu ya kwanza kuja na kioo aina ya AMOLED na FHD+.
Kuhusu bei sifahamu lakini tetesi zinadai simu hiyo haitazidi dolla 400 kwa Tanzania tafadhali tembelea @infinixmobiletz kufahamu lini itatua Tanzania.