Baada ya kampuni ya Infinix kuzindua rasmi simu za Infinix ZERO 6 hapa Tanzania, wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na ufanyaji kazi wa teknolojia ya Artificial intelligent au AI kwenye simu hiyo, hivyo basi leo ningependa kuwajuza namna teknolojia ya AI kwenye kamera za Infinix ZERO 6 inavyofanya kazi.
Pamoja na sifa zingine nzuri za infinix ZERO 6, sifa kuu zaidi ya kwenye simu za Infinix ZERO 6 ni kamera, Infinix Zero 6 imewekewa kamera zenye nguvu sana ambapo kamera za nyuma zinakuja mbili za zenye Megapixel 12 na Megapixel 24. Baada ya majaribio ya kamera hizi ni wazi kuwa simu hizi zinapiga picha bora sana zenye ubora wa hali ya juu. Mbali na kamera za nyuma, kamera ya mbele yenye Megapixel 20 nayo inakuja na uwezo wa kipekee ambapo inaweza kupiga picha bora za Selfie hata kwenye mwanga hafifu.
Na katika kuongeza ubora wa kamera ya Infinix ZERO 6, ndipo teknolojia ya AI inapokuja kufanya kazi sambamba na kamera za simu hii, teknolojia ya AI au Artificial intelligence hutumika kurekebisha kiasi cha mwanga pamoja na rangi ili kufanya picha kuonekana na muonekano halisi. Vilevile teknolojia ya AI kwenye simu hizi inafanya picha kuonekana angavu hata kama eneo husika lina mwanga hafifu.
Vile vile kioo cha Infinix ZERO 6 chanye inch 6.2 kimewekewa ulinzi wa Gorilla glass, hii ikiwa na maana simu hii haitopata michubuko kwenye kioo inapo kuwa mfukoni. Mbali na hayo simu hii pia inakuja na battery yenye uwezo wa 3650 mAh yenye teknolojia ya XCharge kwa ajili ya kuchaji simu hii kwa haraka.
Mbali na kamera, imekuwa ni kama tamaduni kwa Infinix kuzalisha simu zenye muoneka wa kuvutia na safari hii Infinix wamehama kabisa kutoka material ya plastic na metal hadi kwenye aluminium na Class. Infinix imezingatia swala la rangi, kwani inakuja na rangi tatu tofauti Milan Black, Sapphire Cyan na champagne gold, simu hii kwa sasa inapatikana nchi nzima.
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.18 chenye teknolojia ya IPS LCD FHD+ capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz.
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 636 (SDM636).
- Uwezo wa GPU – Adreno 509.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64
- Ukubwa wa RAM – GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 MP, Low-light Sensor na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye 2PD. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Quad LED Flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3650 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Milan Black, Champagne gold na Sapphire Cyan.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Tatizo Hamjaweka bei
Bei ni sh ngapi?