Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Nchini Tanzania

Simu hii inakuja na kioo cha kisasa na kamera nne kwa nyuma
Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Nchini Tanzania Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Nchini Tanzania

Baada ya infinix kuliteka soko na toleo pendwa la Infinix S4, hatimaye kampuni hiyo imezindua rasmi Infinix S5, kinara wa toleo la S series kwa sasa ikiwa na Infinity-O Display na 32MP.

Ujio wa Infinix S5 umeambatana msimu wa sikukuu za Christmas na Mwaka mpya hivyo Infinix imepanga kusherehekea msimu huu kwa kuzindua rasmi promotion itayoanza rasmi tarehe 25/11/2019 na zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio.

Advertisement

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Infinix S5, Afisa wa mahusiano wa kampuni ya Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”.

Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Nchini Tanzania

Vile vile Aisha aligusia kuhusiana na sifa za simu hiyo kwa kusema, “pamoja ya kuwa na selfie kali yenye 32 MP lakini pia inasifa lukuki kama vile teknolojia ya Artificial Intelligence kwenye kamera 4 za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens, lakini pia Infinix S5 ina memory card ya ukubwa wa GB 4 pamoja na uhifadhi wa ndani wa GB 64 yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu nyingi pasipo huitaji ya memory card ya ziada.

Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Nchini Tanzania

Kwa upande wa design Infinix S5 imekuja katika muonekano wa kitofauti wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa ndani ya Display kwa jina la kitaalamu Infinity-O Display na kwa wale wenye matumizi mengi Infinix S5 inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu kutokana na ujazo mkubwa wa Battery wenye mAh 4000”.

Pia kuhusu promotion ya msimu wa sikukuu inayoenda sambamba na uzinduzi wa Infinix S5 meneja wa mauzo wa Infinix Bwana Fredy Kadilana alisema kwamba, katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya Infinix imezindua rasmi promotion inayo wapa nafasi wateja wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na zawadi nyengine nyingi.

Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Nchini Tanzania

Lakini pia Infinix haijasahau wadau wake wa wanaotembelea kurasa za @infinixmobiletz kwa kuitambulisha challenge ya #S5showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii”.

https://www.instagram.com/p/B5DQ7BZHE9C/

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use