Kampuni ya Infinix hivi karibuni inategemewa kuingiza sokoni toleo jipya la simu zake za Infinix Note 6, Simu hii mpya ni toleo jipya la simu ya Infinix Note 5, simu ambayo ilizinduliwa mapema mwaka jana 2018.
Kama ilivyo kawaida ya kampuni ya Infinix, kila mwaka huzindua series mpya ya Infinix Note, simu ambazo zinatengenezwa maalum kwaajili ya watumiaji wanaopenda simu zenye nguvu na uwezo mkubwa. Mwaka huu 2019, Infinix imefanya mabadiliko makubwa ya simu yake hiyo huku ikiwa inakuja na sifa bora pamoja na muonekano wa kisasa zaidi.
Inasemekana kuwa Infinix Note 6 itakuja na kioo cha inch 6.1, kioo ambacho kinasemekana kutengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED pamoja na resolution ya hadi pixel 1080 x 2340. Kwenye kioo hicho kwa juu simu hii inasemekna kuja na kamera ya mbele ya Megapixel 16, kamera ambayo inasaidiwa na teknolojia ya AI ili kupiga picha za selfie vizuri.
Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu, kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 8 na ya mwisho ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote hizi nazo zinakuja na teknolojia ya mpya ya AI pamoja na teknolojia ya AR au Augmented reality.
Take your creativity a notch higher with the Augmented Reality drawing on the Infinix Note 6. Be a genius. #InfinixNote6BeGenius pic.twitter.com/3pOodcqgUj
— Infinix Nigeria (@InfinixNigeria) July 4, 2019
Kwa upande wa sifa Infinix Note 6 inasemekana kuja na processor ya Mediatek MT6765 Helio P35, processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa hadi GB 64, hata hivyo ukubwa huo unaweza kuongezewa kwa kutumia memory card ya MicroSD Card ya hadi GB 500.
Note 6 inakuja na battery yenye uwezo mkubwa wa hadi 4000 mAh, battery ambayo ina uwezo wa kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi yako. Mbali na battery simu hii inakuja na ulinzi wa kutambua uso pamoja na sehemu ya Fingerprint ambayo inapatikana kwa nyuma.
Kwa upande wa bei bado hakuna taarifa kuhusu hilo, ila inasemekana simu hiyo itapatikana kwanza kwa nchini Nigeria pamoja na Uganda na baadae kupatikana kwa nchini Kenya pamoja na Tanzania. Kwa sasa macho yapo kwenye simu mpya ya TECNO Phantom 9 ambayo inategemewa kuzinduliwa hapa Tanzania siku chache zinazokuja.
Unaweza kuangalia hapa chini sifa kamili za simu hiyo mpya ya Infinix Note 6 ambayo tayari imesha zinduliwa hapa Tanzania.
[aps_product_specs id=”33924″]