Ni nini kinahitajika kwa wingi katika eneo maeneo yanayotuzunguka ndio makampuni mengi yanapoonyesha thamani zao kwa wateja wao. Leo nakuletea moja ya kampuni ya simu za mkononi ambayo kupitia bidhaa yake mpya imefanikiwa kufikia wateja wengi sana hasa kutokana na kuwa simu janja imekuwa kama sehemu moja wapo ya eneo la kiofisi.
Kampuni ya simu za mkononi Infinix, mapema mwezi uliopita ilizindua simu za NOTE 40 series ambazo uwekezaji wake mkubwa umefanyika katika teknolojia ya FastCharge. NOTE 40 series kupitia teknolojia ya ‘’All Round FastCharge 2.0’’ na Chip ya Cheetah X1 imebadilisha sura nzima ya simu za daraja la kati.
NOTE 40 Series inajumuisha NOTE 40, NOTE 40Pro na NOTE 40pro+ 5G na kwa ukaribu tutaingalia zaidi NOTE 40Pro. NOTE 40 pro+ inatumia wire wenye fast charge ya Watt 70 kupeleka nishati ya umeme kwenye simu na Magnetic Wireless ya Watt 20 kupeleka nishati ya umeme kwenye simu.
NOTE 40 Series zinamode tatu zakupitisha nishati ya umeme kwenye simu kulingana na hali atakayopendezwa nayo mtumiaji na kulingana mazingira.
Mode ya kwanza ni HYPE mode inapitisha umeme kwa haraka sana kwa muda wa dakika 16 tu simu inaijaza kwa asilimia 50% hii husaidia pale unapokuwa kwenye hali ya haraka na ungependelea simu ipate charge kwa haraka, Mode ya pili ni SMART mode hii inaruhusu simu kujaa charge kwa muda wa dakika 20 tu na Model ya tatu ni TEMP Mode kazi yake kubwa ni kushusha joto la simu inapokuwa imetumika kuchakata kazi nyingi na inahiitaji kuingia chaji ikiwa katika hali ya hali joto.
Pamoja na mode hizo tatu lakini pia simu hizi zinanjia nyengine za kumfanya mtumiaji aendelea kufurahia simu miongoni mwa njia hizo hii ya Bypass, Reverse, AI Charging protection, Extreme Charging -20C. kupitia teknolojia hizi zinampa mtumiaji uhakika wa kuwa hewani muda wote hata pale endapo simu inaonyesha ishara yakuishiwa charge bado anaweza kuendelea kuitumia huku ikiwa kwenye charge pasipo madhara yoyote.
AI Charging protection kazi yake kubwa ni kuujua muda ambao mtumiaji anacharge simu yake mfano kama mara nyingi inaicharge simu yako nyakati za usiku basi Ai protection itailinda kwa kuruhus umeme kuingia kwa asilimia 80% na kumaliza 20% asubuhi.
Reverse Charging inaweza kufanyaika kwa kutumia wire ambapo kupitia wire umeme utasafirishwa kwa kutumia watt 10 na bila wire yani kwa kuigusanisha NOTE 40 series na simu nyengine umeme utasafirishwa kwa watt 5.
Kwa mujibu wa Infinix wenyewe ni kuwa battery ya NOTE 40 Series ambayo ni mAh5000 inauwezo kwa kupokea charge mizunguko zaidi 1600 pasipo kupoteza ufanisi.
Muongozo mzima huu wa kupitisha charge kwa haraka, kutunza charge na kutoa ulinzi kwenye mfumo mzima wa charge unasimamiwa na chip aina ya Cheetah X1, chip ambayo ni tengenezo la kampuni ya Infinix.
Kwa ufupi Note 40 series ndio simu pekee zenye teknolojia ya fastcharge ambayo inapatikana kwa bei rafiki kama ambavyo lengo la Infinix ni kumshika mkono kila kijana kufikia ndoto zake kupitia teknolojia.