Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Infinix Note 40 Kupokea Mfumo Mpya wa Android Hadi Android 16

Mabadiliko hayo yataanza kuonekana katika simu mpya za Infinix NOTE 40
Infinix Note 40 Kupokea Mfumo Mpya wa Android Hadi Android 16 Infinix Note 40 Kupokea Mfumo Mpya wa Android Hadi Android 16

Kampuni ya simu za mkononi Infinix imeuimarisha mfumo wake wa uendeshaji/Operating system ‘XOS’ na mabadiliko hayo yataanza kuonekana katika simu mpya za Infinix NOTE 40.

Simu za NOTE 40 kuja kupokea Android version upgrade mbili na security upgrade kwa muda wa miezi 36 duniani kote. Infinix inatambua umuhimu wa maisha marefu ya programu na imejitolea kuwapa watumiaji hali ya utumiaji thabiti, laini kwa muda mrefu. Hili linaashiria mabadiliko makubwa ya mbinu za kampuni.

Advertisement

NOTE 40 Pro, NOTE 40 Pro 5G, NOTE 40 Pro+ 5G, kuja na Android 14, ikiwa na mipango ya kupata toleo jipya la Android 16. Hii ina maana kwamba watumiaji kutarajia mfumo wa XOS usiliolaini na unaotegemeka kwa muda mrefu na kuhakikisha maisha marefu ya vifaa vyao.

Mkakati huu kuja kubaddilisha mtazamo wa simu za bei ya kati katika soko, ambapo mara nyingi huwa nyuma katika upokeaji wa update za software na hili kuzifanya simu za NOTE 40 kuwa simu yenye teknolojia bora zaidi kupatikana kwa bei rafiki.

Infinix imejidhatiti kuweka upgrade ya programu za software kuwa na muda mrefu kuridhisha wateja na kuonyesha ubunifu. Mbali na uboreshaji wa programu, mfululizo wa NOTE 40 Pro unaangazia All-Round FastCharge 2.0.

kiendeshwa na chipu ya iliyojitengenezea na Infinix, Cheetah X1, NOTE 40 kutoa hali nzuri ya kuchaji, ikijumuisha chaji ya waya ya 100W kwa haraka sana, kuchaji bila waya kwa sumaku/magnetic charge na chaguzi za kuchaji kwa kasi nyingi. Uwezo huu wa hali ya juu wa kuchaji unakidhi mahitaji ya watumiaji wenye ujuzi wa teknolojia.

Upatikanaji wa Android version upgrade unaweza kutofautiana katika vifaa na maeneo mbalimbali kutokana na vikwazo mbalimbali vya udhibiti.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use