Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023)

Fanya uchaguzi kwa kuangalia tofauti ya Infinix NOTE 30 Pro na Galaxy A34
Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023) Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023)

Katika ulimwengu wa simu za mkononi, Infinix Note 30 Pro na Samsung A34 ni simu mbili zenye ubora kulingana na mahitaji yako ya mwaka 2023. Simu zote mbili zina sifa na features kulingana na mahitaji yako.

Hata hivyo, uchunguzi wa karibu unaonyesha kuwa Infinix Note 30 Pro ni simu bora zaidi kwa mwaka 2023 ikilinganishwa na simu ya Samsung, haswa kwa wale wanaotamani utendaji bora na teknolojia mpya zaidi pamoja na mfumo mpya ambao sisi tunaita #GusainishaIjae.

Advertisement

Kioo

Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023)

Infinix Note 30 Pro ilitangazwa tarehe 16 Mei 2023, na kuja na huduma kadhaa muhimu. Ina kioo kikubwa cha inch 6.78 AMOLED, kikiwa na resolution ya FHD+ yaani pixel 1080 kwa 2460, kioo ambacho ni kubwa kuliko kioo cha Samsung A34 chenye inch 6.6. Kioo cha Note 30 Pro pia kinakuja na refresh rate ya juu ya 120Hz ili kusaidia kutumia apps na game kwa urahisi zaidi.

Utendaji

Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023)

Kwa utendaji, Infinix Note 30 Pro inatumia processor ya MediaTek Helio G99 ultra-power, iliyotengenezwa kwa teknolojia ya 6nm, na kasi ya processor inayofikia 2.2 GHz. Hii inaambatana na RAM iliyozidishwa hadi 16GB na uhifadhi wa 256GB.

Kwa upande mwingine, Samsung A34 inatumia chipset ya MediaTek MT6877V Dimensity 1080 yenye CPU ya octa-core na inatoa hadi RAM ya 8GB na uhifadhi wa 256GB. Note 30 Pro inazidi kuwa bora kutokana na uwezo wake wa RAM wa juu, hivyo uwezo huu utafanya uweze kutumia simu hii kwa haraka zaidi kuliko Galaxy A34.

Kamera

Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023)

Kwenye idara ya picha, Note 30 Pro pia inaonekana kuwa bora zaidi kwani ina mfumo wa kamera kuu ya 108 MP pamoja na kamera ya kina ya 2 MP na kamera ya makro ya 2 MP, na kamera ya selfie ya 32 MP. Hii ni tofauti kubwa kutoka kwa mfumo wa kamera ya Galaxy A34 yenye MP 48 na kamera ya selfie ya MP 13. Kwa Note 30 Pro, watumiaji wanaweza kutarajia picha zenye rangi nyingi na muonekano bora zaidi.

Battery (#GusainishaIjae)

Simu zote mbili zina betri yenye uwezo wa 5000 mAh, ikitoa nguvu ya kutosha kwa matumizi ya siku nzima. Hata hivyo, Note 30 Pro inaongoza na uwezo wake wa fast charging ya hadi 68W.

Simu Bora Kati ya Infinix NOTE 30 Pro vs Galaxy A34 (2023)

Mbali ya hayo Infinix Note 30 Pro inakusogezea ulimwengu mpya #GusainishaIjae ambapo sasa simu mpya ya Infinix NOTE 30 Pro inakuja na uwezo wa kuchaji simu nyingine kwa kugusanisha na simu ya nyingine yenye wireless charging. Sehemu hii husaidiwa na teknolojia ya reverse wireless charging yenye uwezo wa hadi 15W.

Kwa upande mwingine simu ya Galaxy A34 inakuja na fast charging ya 25W. Huku ikiwa haina teknolojia ya kuchaji simu nyingine. Hii inafanya Infinix Note 30 Pro kuchaji kwa haraka ndani ya muda mfupi, ambao ni faida kubwa kwa wale ambao wana haraka ya kupambana na Maisha.

Bei

Bei ni moja kati ya sehemu muhimu kuangalia hasa kama unataka kununua simu kwa mwaka huu 2023, kwa upande wa bei Galaxy A34 inapatikana kwa bei ya kuanzia TZS 700,000 bei hii inaweza kuongezeka kulingana na mahali utakapo nunulia simu hiyo, huku kwa Infinix Note 30 Pro unaweza kupata sifa zote ikiwa na mfumo wa #GusainishaIjae kwa TZS 650,000 Tu

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use