Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Infinix NOTE 12 VIP na Galaxy S22 Ultra Kufanana Megapixels

Infinix NOTE 12 VIP inakamera tatu nyuma na Kamera kuu imebeba Megapixel 108
Infinix NOTE 12 VIP na Galaxy S22 Ultra Kufanana Megapixels Infinix NOTE 12 VIP na Galaxy S22 Ultra Kufanana Megapixels

Je unafahamu kampuni ya simu Infinix imezindua rasmi simu ya kwanza ya watt 120?, Mei 16/5/2022 Kampuni ya simu za mkononi Infinix ilizindua rasmi Matoleo matatu ya mfululizo wa series ya NOTE – Infinix NOTE 12 VIP, NOTE 12 PRO na NOTE 12.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka mitandaoni, Infinix imejibebea sura mpya baada ya ujio wa matoleo haya ya NOTE huko ugaibuni.

Advertisement

Infinix NOTE 12 VIP na Galaxy S22 Ultra Kufanana Megapixels

Infinix NOTE 12 VIP ina feature zenye teknolojia ya hali ya juu na moja kati ya features zilizoshangaza na kuwavutia wengi ni watt 120 ya USB ilivyo na nguvu ya kuchaji simu hiyo ya battery la ukubwa wa mAh 4500 100% ndani ya dakika 17 tu.

Infinix NOTE 12 VIP na Galaxy S22 Ultra Kufanana Megapixels

Infinix NOTE 12 VIP imebeba maana halisi ya VIP kwa namna mbili, moja ni namna simu hii ilivyofaulu kwa nafasi kubwa upangiliaji na uwasilishaji wa kila feature yenye kuunda simu hii. Infinix NOTE 12 VIP inakamera tatu nyuma na camera kuu imebeba Megapixel 108.

Hii ni mara ya kwanza kwa toleo la NOTE kuja na qualiti hii ya camera, Camera ya NOTE 12 VIP ina uwezo mkubwa wa kuchukua video kwa slow motion kwa resolution 720p/HD na programme ya uchukuaji yenye kasi ya nyuzi 120 ambayo ni sensor kali na kubwa pia ilitumiaka katika simu aina ya Samsung Galaxy S22 Ultra.

Haya ni mapinduzi makubwa ya teknolojia ya simu kuwahi kufanyika na kampuni hii, Infinix imekuwa imara kwa kila toleo jipya na unaweza kuona tofauti kubwa kati ya matoleo ya awali na mapya kwa kugusia sifa hizi chache unaweza kusema Infinix NOTE 12 VIP ni Zaidi ya mara tatu ya Infinix NOTE 11, Infinix, NOTE 11 inatumia chaji ya watt 33 na megapixel 64 ikiwa ndio camera kuu.

Swali ni je hii NOTE 12 VIP ya ugaibuni ndio itakayotua bongo na kama ni hivyo simu hii itapatikana nchini kwa shillingi ngapi za kitazania? Shusha maoni yako kuhusu simu hii @infinixmobiletz

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use