Kuanzia mwezi wa October hadi Novemba tumeona Makampuni mengi ya simu za mkononi yakiiingia katika ushindani mkubwa katika soko la simu.
Kutokana na kuwepo kwa matoleo mengi mapya ya simu ambayo yameingia kwa kipindi kimoja mimi safari yangu leo ni kukujuza kuhusu moja ya toleo jipya la simu aina ya Infinix NOTE 11 pro ambayo ilizinduliwa rasmi nchini Tanzania Novemba hii.
Pasipo kupoteza muda tutaangalia moja kwa moja kuhusu sifa za simu hii na kisha utafahamu kwanini nimetamani na wewe uifahamu simu hii.
Infinix NOTE 11 pro inafahamika kama simu ya kwanza ya Android kati ya simu zinazotumia Chipset processor aina ya Mediatek Helio kuwa ya kwanza kuhamia kwenye speed ya juu zaidi ambayo ni MediaTek Helio G96 ikiambatana na features nyingine zenye kuashiria ongezeko la speed katika simu hii ambazo ni refresh rate ya nyuzi 120Hz, Ram ya GB 8 kwa jumuisha Ram ya ziada ya GB 3 Pamoja na Monster Game kit.
Zile shida za simu kustuck, kupata moto na kuzima hafla sahau kabisa haijalishi NOTE 11 pro utaipigisha mzigo kwa kiasi gani sababu Infinix NOTE 11 pro inawalenga zaidi watu wa namna hiyo ambao kwao simu ni sehemu ya ofisi au kwa mwanafunzi tunaweza sema darasa na kwa wapenzi wa entertainment ni kama sehemu ya kiburuidisho. Infinix NOTE 11 pro inaweza kutype, kuedit, kuscan, kufanyia presentation, kucheza games za aina zote nk.
Feature nyengine ya simu hii ambayo ni mkombozi wa wengi ni kuhimili kudumu na chaji kwa siku zaidi ya moja na matumizi mengine ya mtandaoni yakiendelea kama kawaida.
Infinix NOTE 11 pro ina mAh5000 na 33 Wh ya fast charging lakini pia bado ikumbukwe inaprocessor yenye speed hivyo hizi feature tatu zinapo fanya kazi kwa pamoja unyo nywaji wa battery unakuwa mdogo sana na kujaa kwa chaji ni kwa haraka sana.
Tukija kwenye swala zima la picha Infinix NOTE 11 pro ina kamera 3 nyuma na Kamera kuu ni Megapixel 64 na kamera za ziada ni Megapixel 13 kwa 2. Megapixel 13 ni kwaajili ya telescope zooming ambapo unaweza kuzoom mara 30X ili kabla ya kuchukua picha.
Kamera ya mbele ni Megapixel 16 na uzuri zaidi inaprogram nyingi sana za kukufanya wewe uwe vile ungependa pasipo haji ya kudownload application za urembo. Teknolojia ya AI inafanya kazi nyingi sana ukiwemo ku-switch kamera kwenda na uhalisia wa mazingira.
Vile vile mfumo wa kuendesha simu ni XOS Android 11. Infinix imejitahidi kuongeza theme na wepesi wa simu kuweza kuteleza vizuri wakati wakuscroll lakini pia unaweza amua kutumia mfumo wa Vertical au Horizontal.
Infinix NOTE 11 pro zinapatikana katika maduka yote ya simu inchini Tanzania zikiwa na ofa ya GB 96