Kampuni ya simu za mkononi Infinix yazindua rasmi Infinix NOTE 11 na NOTE 11 pro kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano Tigo Tanzania.
Infinix NOTE 10 na NOTE 10 ni simu za kwanza kwa kampuni ya simu Infinix kuja na processor ya MediaTek Helio G96 na AMOLED Display ya inch 6.7 FHD+. Infinix imelenga kurahisisha utendekaji wa kazi kwa haraka zaidi na ubora zaidi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya simu hizo mbili. Kampuni ya Infinix na Tigo wamekuwa washirika wa muda mrefu sana. Infinix ikijaribu kuja na matoleo bora kwa bei rafiki na Tigo ikijaribu kutoa ofa mbalimbali ili kuongeza wimbi la watumiaji simu janja na kupunguza gharama za uendeshaji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix imekuwa ikimpa sababu mfanya kazi wa sector mbalimbali kuweka Imani kubwa kwenye teknolojia ya simu kwa ambavyo inaweza kumrahisishia kazi zake kwa haraka zaidi. Naitambulisha kwenu Infinix NOTE 11 pro kama chombo muhimu chenye kufanya kazi kwa waledi kutokana na sifa hizi Chipset ya MediaTek Helio G96 inayofanya kazi sambamba na refresh rate ya 120Hz katika kuongeza wepesi na speed wakati wa kucheza games na kazi nyengine za kiofisi”
Aliongeza “Infinix inakupa chaguzi ya kumiliki kile kinachoendanana mazingira yako ya kazi Infinix NOTE 11 ni simu ya kwanza ya toleo la NOTE kuja na kioo cha aina ya AMOLED chenye faida kubwa kwa mtumiaji kutokana na kuwa na unyonyaji mdogo wa chaji lakini pia huonyesha picha zikiwa katika rangi halisi kuendana na mazingira husika”.
Mkakati wetu ni kuharakisha kupenya kwa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi ya 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa GB96 za internet bure kwa mwaka mzima ili wateja wote wa Infinix NOTE 11 na NOTE 11 pro wajifunze mengi pasipokuwa na gharama, alisema Mkuu wa Maduka na bidhaa Tigo Bwana Mkumbo Mnyonge.
Baadhi ya sifa nyengine za simu hizo ni battery ya ujazo wa mAh5000 yenye fast charge ya Wh 33 na kamera yenye zoom lens 30X, Kujua mengi zaidi Tembelea maduka ya Tigo na Infinix.