Kampuni ya Inifnix hivi karibuni inaweza kuzindua simu mpya ya Infinix Note 10 Pro ambayo kwa sasa inasemekana ipo kwenye hatua za awali.
Kwa mujibu wa ukurasa wa majaribio ya simu wa geekbench Infinix Note 10 Pro imeonekana ikiwa inatumia chipset ya MediaTek Helio G90T pamoja na RAM ya GB 8.
Kwa upande wa matokeo ya majaribio kwenye ukurasa wa geekbench, Infinix Note 10 Pro inaonekana kuwa na point 433 kwa majaribio ya single-core na point 1,125 kwa majaribio ya multi-core. Majaribio hayo pia yanaonyesha Infinix Note 10 Pro itakuja ikiwa inatumia mfumo wa Android 11.
Kwa upande mwingine, simu hii pia imeonekana kwenye ukurasa wa tovuti ya FCC ambapo kupitia ukurasa huo simu hiyo inasemekana kuja na uwezo wa 5G, uhifadhi wa ndani au ROM ya GB 256 pamoja na uwezo wa teknolojia ya fast charging ya hadi 33w.
Kwa sasa bado hakuna tarehe maalum ambayo simu hii inaweza kuzinduliwa rasmi lakini pengine tegemea kusikia zaidi kuhusu simu hii kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu 2021. Kwa taarifa zaidi kuhusu simu hii mpya ya Infinix Note 10 Pro na simu nyingine za Inifnix endelea kutembelea Tanznaia tech kila siku.