Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Infinix Hot S4 Kuzinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Tarehe 14 May

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kwa kushirikiana na kampuni ya Tigo Tanzania
Infinix Hot S4 Kuzinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Tarehe 14 May Infinix Hot S4 Kuzinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Tarehe 14 May

Kampuni ya Infinix imetuma mialiko mbalimbali kwa wapenzi wa simu zake za Infinix kuhudhuria kwenye tamasha la uzinduzi wa simu mpya ya Infinix Hot S4 itakayo zinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza hapa nchini Tanzania.

Infinix Hot S4 ni moja kati ya simu bora sana kutoka kampuni ya Infinix na pia ni simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo yenye kuja na kamera tatu kwa nyuma. Mbali na hayo simu hiyo inakuja na muonekano wa kisasa pamoja na sifa bora.

Advertisement

Infinix Hot S4 Kuzinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Tarehe 14 May

Hot S4 inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Kioo hicho kwa mbele kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama waterdrop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya mbele yenye Megapixel 32.

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu ambazo hizi zina uwezo wa Megapixel 13, Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, kamera zote za nyuma zinasaidia na flash ya Quad-LED flash na teknolojia ya AI ambayo inasaidia kufanya picha ziwe na muonekano mzuri. Unaweza kusoma hapa ili kujua sifa kamili za Infinix Hot S4.

Hot S4 inatarajiwa kuzinduliwa hapa Tanzania siku ya Jumanne ya tarehe 14 mwezi wa tano, ambapo tamasha la uzinduzi linatarajiwa kufanyika ndani ya Hotel ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam kuanzia mida ya ya saa 12 jioni hadi saa 3 ya usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Infinix Hot S4 Kuzinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Tarehe 14 May

Endelea kuwa nasi tutakuletea yote yatakayo jiri kwenye uzinduzi huo utakao fanyika siku ya jumanne ya wiki ijayo hapa Dar es salaam.

Mbali na hayo kampuni ya Tecno ambayo ni brand ya kampuni moja pamoja na Infinix, hapo jana tarehe 8 mwezi wa tano kwa kushirikiana na kampuni ya kutoa huduma za simu ya Tigo Tanzania imezindua rasmi simu zake mpya ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro.

Infinix Hot S4 Kuzinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Tarehe 14 May
Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog

Hata hivyo kupitia uzinduzi huo wateja watakao nunua simu hizo mpya za Tecno, wataweza kufurahia huduma ya mtandao wa Internet wa Tigo pamoja na kifurushi cha GB 96 bure watakachoweza kutumia kwa muda wa mwaka mzima. Unaweza kusoma hapa kujua sifa kamili pamoja na bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use