Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Mpya ya Infinix Hot S4 Yazinduliwa Rasmi Nchini Kenya

Hatimaye Simu mpya za Infinix Hot S4 zimefika nchini Kenya
Simu Mpya ya Infinix Hot S4 Yazinduliwa Rasmi Nchini Kenya Simu Mpya ya Infinix Hot S4 Yazinduliwa Rasmi Nchini Kenya

Kampuni ya Infinix hivi leo imezindua rasmi simu mpya za Infinix Hot S4, simu hizi zimezinduliwa hivi karibuni nchini Nigeria na huwenda siku za karibuni zikaja hapa nchini Tanzania.

Akiongea kwenye uzinduzi wa simu hiyo huko nchini Kenya, Livingston Migwi ambaye ni meneja wa maendeleo ya biashara wa kampuni ya Transsion ambayo ndio kampuni mama ya brand za Inifnix na Tecno amesema kuwa, brand ya infinix kwa sasa inazidi kukuwa sio tu kwenye mipaka ya Afrika, bali sasa brand hiyo imesha anza kujulikana kwenye nchi za Asia ya Mashariki, Indonesia Dubai na UAE au Falme za Kiarabu.

Advertisement

Simu Mpya ya Infinix Hot S4 Yazinduliwa Rasmi Nchini Kenya

Kama bado hujafanikiwa kusoma sifa za Infinix Hot S4, Simu hii inakuja na kamera tatu ambazo hizi zina uwezo wa Megapixel 13, Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, kamera zote za nyuma zinasaidia na flash ya Quad-LED flash na teknolojia ya AI ambayo inasaidia kufanya picha ziwe na muonekano mzuri.

Kwa upande wa processor, simu hizi zinaendeshwa na processor ya Mediatek’s Helio P22 SoC ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 kwa infinix Hot S4 na GB 6 kwa Infinix Hot S4 Pro, matoleo hayo pia yanatofautiana kwenye ukubwa wa ROM kwani Hot S4 inakuja na ROM ya GB 32 na Hot S4 Pro inakuja na ROM ya GB 64. Ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi GB 128. Sifa kamili za Infinix Hot S4 na Hot S4 Pro unaweza kusoma hapa.

Kwa upande wa bei nchini Kenya Infinix Hot S4 inatarajiwa kuuzwa kwa Shilingi za Kenya Ksh 14,999 (Tsh 344,000) kwa toleo lenye ROM ya GB 32, na kwa toleo lenye GB 64 kama uko nchini Kenya tegemea kuipata kwa Shilingi za Kenya Ksh 18,999 (Tsh 436,000).

Kwa sasa bado simu hizi hazijafika hapa nchini Tanzania pengine ni kwa sababu kampuni ya Tecno hapa nchini Tanzania inajiandaa na uzinduzi wa simu mpya za Tecno Camon, simu ambazo pia zimesha zinduliwa siku kadhaa zilizopita huko nchini India. Kujua pindi simu hii itakapo fika hapa Tanzania hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use