Kampuni ya Apple Yatangaza Matoleo Mapya ya iPad na iPhone

Kwa mara ya kwanza kampuni ya Apple yaleta iPad na iPhone za rangi nyekundu
iPad na iphone iPad na iphone

Mapema leo kampuni ya Apple ilifunga kurasa zake za tovuti ya apple.com na kuweka tangazo linalo ashiria ujio wa bidhaa mpya, masaa machache yaliopita tovuti hiyo ilifunguliwa huku ikiwa na tangazo linalo onyesha ujio wa iPad na iPhone mpya za rangi nyekundu.

Kampuni hiyo inasemekana kuwa imefanya maboresho kadhaa kwenye simu hizo pamoja na kuleta iPad mpya ya inch 9.7. Habari kutoka kwenye mtandao wa thenextweb zinasema kuwa kuletwa kwa simu hizo za rangi nyekundu ni katika kuendeleza kupinga maambukizi ya HIV kampeni ambayo ilizinduliwa na Apple baada ya kampuni ya hiyo kuungana na taasisi ya RED ambayo lengo lake ni kupinga na kupiga vita mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi au HIV.

Advertisement

Kuhusu simu hizo iphone 7 hiyo mpya ya rangi nyekundu itakuwa na sifa zilezile za kawaida lakini tofauti yake ni kuwa itakuja kwa rangi nyekundu na ituzwa kwa dollar za marekani $749 huku ile ya inch 4.7 itauzwa kwa dollar za marekani $869. Kwa upande wa iPad simu hiyo inakuja na kioo chenye teknolojia ya Retina na ukubwa wa inch 9.7 huku ikiwa na resolution ya 2048×1536 pamoja na processor ya 64 bit 9 Chip huku ikiwa na uwezo a kudumu na chaji kwa masaa 10 kama ikichaji ikajaa kabisa. Kuhusu bei ipad hiyo mpya itauzwa kwa bei nafuu ya dollar za marekani $329 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 740,000.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use