Kampuni ya simu ya Infinix Mobile yenye Makao Makuu Hong Kong imebuka kidedea baada ya toleo mama la kampuni hiyo Infinix ZERO kujinyakulia tuzo ya nidhamu kwenye kitengo cha bidhaa bora ya mawasiliano yenye muonekano wakuvutia zilizotolewa na IF DESIGN kwa mwaka huu wa 2021.
Infinix ZERO 8 ilishinda baraza la washiriki 98 linaloundwa na wataalamu wakujitegemea kutoka ulimwenguni kote, design ya Infinix ZERO 8 iliyotawaliwa na mzunguko wa kioo na chuma, sifa nyengine zilizoifanya Infinix ZERO 8 kuibuka kinara ni display ya nch 6.85 FHD+ camera yenye uwezo wa kunasa matukio kila pembe.
Ushindani ulikuwa ni mkubwa takribani nchi 52 ziliweka muhuri wa kukubalia Infinix ZERO 8 ndio simu bora kwenye kipengele cha nidhamu ya mawasiliano baada ya kuyapiga chini makampuni mengine ya simu.
IF DESIGN huandaliwa kila mwaka na shirika la ubunifu ulimwenguni Hannover-based If international Forum Design GmbH.
Tuzo za IF DESIGN ni tuzo zenye kujumuisha bidhaa zote zenye muonekana wa kuvutia, kipekee na imara. IF DESIGN imekuwa ikitoa tuzo hizi kwa kupambanisha bidhaa kwenye taaluma zifuatazo nidhamu, ufungashaji (packaging), ubunifu wa huduma, usanifu na usanifu wa mambo ya ndani pamoja na dhamana ya utaalamu.
Na msemo wake wa THE FUTURE IS NOW, Infinix inakusudia kuwapa nguvu vijana wa leo kujitokeza katika um ana kuonyesha ulimwengu wanachokiamini na kukisimamia.
Bidhaa za Infinix zinapatikana zaidi ya nchi 40 ulimwenguni, zikijumuisha Afrika, Amerika kusini, Mashariki ya kati na Kusini mwa Asia.
Infinix kwa mwaka wa 2018-2020 imekuwa kwa kasi ya 160% kiasi cha kushangaza na huku kila leo ikija na mikakati mbalimbali kufikia watu wengi zaidi kupitia matangazo ya mitandaoni na uzalishaji wa simu zenye teknolojia ya hali ya juu.
Soma Zaidi Hapa – IF DESIGN