Kipindi cha nyuma kidogo wakati kabla Samsung haijazindua simu zake mpya za Galaxy S9 na S9 Plus, tulisikia tetesi za ujio wa toleo la tatu la simu ya Galaxy S9 Lite au S9 Mini. Kutoka kipindi hicho hadi sasa bado tetesi za ujio wa simu hii zina endelea na baadhi ya tovuti mbalimbali tayari zimeanza kutoa ripoti uhenda huu ndio muonekano wa simu hiyo.
Kwenye video hapo juu ni simu iliyo pewa jina la Samsung Galaxy A9 Star (G8850), simu hii ndio inasemekana kuja kwa jina hilo, lakini kama ilivyokuwa kwenye simu ya Samsung Galaxy S8 Lite ambayo nayo ilipewa jina la tofauti na kuitwa Samsung Galaxy S Light Luxury, inasemekana pia nayo Galaxy S9 Lite itakuja na jina la tofauti lakini sifa zitakuwa zinafanana kabisa na Galaxy S9.
Simu hii inategemea kuja na kioo chenye ukubwa wa inch 6.28 chenye teknolojia ya super AMOLED ambacho pia kita kuwa na resolution ya 1,080 x 2,220. Kwa mujibu wa tetesi hizo simu hio pia inategemea kuja na battery ya 3,700 mAh ambayo pia itakuja na teknolojia ya Fast Charge.
Kuhusu kamera najua hata wewe umeshangaa muundo wa kamera za simu hii kwani kama unavyo ona hii ni simu ya kwanza kwa Samsung mwaka huu kuwa na kamera ambazo ziko pembeni kwa mtindo huo. Kamera hizo zinategemewa kuwa na uwezo wa megapixel 24 na nyingine inasemekana kuwa na Megapixel 16. Kamera ya mbele inasemekana kuwa na kamera yenye uwezo wa Megapixel 24.
Mbali na hayo Galaxy A9 Star (G8850) a.k.a (Galaxy S9 Lite) inasemekana kutumia mfumo wa uendeshaji wa Android 8.0 ambao utakuwa ukisaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 huku ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa memory card.
Kwa sasa bado hakuna ripoti kamili kuhusu tarehe ya ujio wa simu hii, kwa habari zaidi kuhusu simu hii na upatikanaji wake endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa habari kamili kuhusu sifa kamili za simu hii, bei na upatikanaji wake kwa hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
Iko poa sana hii simu dooh