Hatimaye YouTube Yaja na Huduma Mpya ya YouTube Music

Sasa utaweza kusikiliza na kuangalia muziki kwenye sehemu moja
Hatimaye YouTube Yaja na Huduma Mpya ya YouTube Music Hatimaye YouTube Yaja na Huduma Mpya ya YouTube Music

Mwishoni mwa mwaka jana 2017 tulitoa taarifa za kuhusu ujio wa huduma mpya ya YouTube Music, Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hivi karibuni huduma hiyo imetangazwa kuanza rasmi. Kwa mujibu wa blog ya YouTube, huduma hiyo mpya ya YouTube Music itakuwa ni kwaajili ya muziki pekee na itakuwa na nyimbo mbalimbali za wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

YouTube Music pia itakuwa na chati mbalimbali za muziki, album za muziki za wasanii, maonyesho ya mubashara ya wasanii, playlist, nyimbo za kurudiwa (cover songs) pamoja na video mbalimbali za muziki.

Advertisement

YouTube Music itakuwa inapatikana kupitia tovuti na App mpya ya YouTube Music ambayo ita-anza kupatikana hivi karibuni. Mbali na hayo huduma hii mpya itakupa uwezo wa kusikiliza na kuangalia nyimbo mbalimbali bure huku ikiwa na matangazo, Pia unaweza kutumia huduma ya YouTube Music Premium kwa kulipa dollar $9.99 kwa mwezi sawa na Tsh 22,900 kwa mwezi ili kutumia huduma hiyo bila matangazo huku ukiwa na uwezo wa kupakua nyimbo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza pale unapokuwa huna internet.

Hata hivyo Youtube imetangaza kuwa, huduma hiyo itaanza kupatikana kuanzia tarehe 22 mwezi huu kwa nchi za Marekani, Australia, New Zealand, Mexico na Korea ya Kusini. Baadae kwenye awamu ya pili huduma hiyo itapatikana kwa nchi za Austria, Canada, Denmark, Finland, France, Germany, Ireland, Italy, Norway, Russia, Spain, Sweden, Switzerland pamoja na United Kingdom. Kwa sasa kama uko kwenye nchi za Afrika pamoja na nchi nyingine ambazo haziko kwenye list hiyo, unaweza kujisajili ili kupata taarifa pindi huduma hiyo itakapo anza kupatikana kwenye nchi uliyopo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use