Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Google Yatangaza Huduma Mpya ya Youtube TV

Kaa tayari kwa huduma mpya kutoka google ya youtube TV
YOUTUBE TV YOUTUBE TV

Katika mkutano wa Google uliofanyika leo huko california nchini marekani kampuni hiyo ilitangaza kuleta huduma mpya ya Youtube TV, huduma hii itaweza kuleta uwezo wa watumiaji wa huduma hiyo kuona channel mbalimbali zenye kuonyesha Tamthilia, filamu, michezo na burudani mbalimbali.

Ili kuweza kutumia huduma hiyo utaitajika kulipia dollar za marekani $35 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 80,000 kila mwezi ili kuendelea kutazama burudani hizo kupitia Youtube TV. Huduma hiyo pia inakuja na sehemu inayoitwa Cloud DVR ambayo inakuwezesha kuhifadhi vipindi na burudani mbalimbali bila kuwa na mipaka yani Unlimited, lakini kumbuka ili kuangalia vipindi ulivyo hifadhi inakubidi kuwa na internet kwenye simu au kompyuta yako. Kwa sasa Youtube TV inakuja na channel mbalimbali angalia hapo chini kujua channel zilizopo kwenye huduma hivyo mpya.

Advertisement

Kwa sasa huduma hii bado haijafika kwa hapa Tanzania lakini dalili za huduma hii kuja Tanzania ni kubwa sana, unaweza kujua zaidi kupitia tovuti ya huduma hiyo hapa. Pia unaweza kuendela kujua kuhusu huduma hii kwa kutembela Tanzania Tech kila siku kwani tutaendelea kukuhabarisha pindi tutakapo jua chochote kuhusu huduma hii mpya kutoka Google.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use