Kampuni ya Huawei kupitia mkutano wa MWC 2018 imetangaza laptop yake mpya ambayo ni toleo jipya la Laptop ya mwaka ya Huawei Matebook X, Laptop hii mpya ya Huawei Matebook X Pro inakuja na muonekano mpya pamoja na sehemu mpya mbalimbali za ulinzi.
Laptop hii mpya ya Huawei Matebook X Pro inakuja na machaguo mawili ya processor ikiwa ni pamoja na processor ya 7th-gen Intel Core i5 pamoja na processor ya Core i7 CPU. Kwa upande wa RAM laptop hii inakuja na machaguo mawili ikiwa ni pamoja na laptop yenye RAM ya GB 8 pamoja na nyingine yenye RAM ya 16, Hard Disk ya laptop hii pia zinakuja za aina mbili moja ikiwa na ukubwa wa GB 256 ya mfumo wa SSD pamoja na nyingine ya GB 512 nayo pia ya mfumo wa SSD, kwa upande wa mfumo wa uendeshaji Huawei Matebook X Pro inakuja ikiwa inatumia toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa Windows 10.
Tukiangalia upande wa Graphics, Huawei Matebook X Pro inakuja na Graphics Card ya Nvidia GeForce MX GDDR5 yenye uwezo wa GB 1502. Tukiamia kwa upande wa sehemu za viunganishi, Laptop hii mpya kutoka Huawei inakuja na sehemu mbili za kuchomeka USB za aina ya Type-A USB pamoja na sehemu moja ya kuchomeka USB ya Type-C USB. Vilevile tukiangalia upande wa sauti Laptop hii inakuja na mfumo wa sauti wa Quad-speakers wenye teknolojia ya Dolby Atmos.
Bei pamoja na siku ya kupatikana kwa laptop hii bado haija julikana (Bado hawaja tangaza). Ili kujua lini laptop hii mpya itaingia sokoni pamoja na mahali pa kuipata kwa hapa Tanzania endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yote hapa hapa.