Kampuni maarufu ya teknolojia ya Huawei hapo jana ilizindua simu yake mpya ya Huawei Mate 9, simu hiyo iliyozinduliwa huko nchini ujerumani ni moja kati ya simu kubwa kuliko zote kutoka kampuni hiyo yenye makao makuu yake yaliyoko Shenzhen nchini China.
Simu hiyo mpya ya Huawei Mate 9 inayo kioo chenye ukubwa wa inch 5.9 ikiwa na teknolojia ya FHD display yani (Full High Definition Display), simu hiyo pia inaendeshwa na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android Nougat 7.0 pamoja na processor ya Kirin 960 octa-core ikiwa na RAM ya 4GB. Kuhusu ukubwa (storage) ya simu hii, Huawei Mate 9 inayo storage ya ndani ya GB 64 pamoja na sehemu ya microSD slot ambayo inatumika kuongeza ukubwa (storage) ya simu hiyo.
Pia Huawei Mate 9 inatumia Network za GSM / CDMA / HSPA pamoja na LTE au 4G, vilevile simu hii inatumia WiFi connectivity, fingerprint reader pamoja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 20 na nyingine ikiwa na Megapixel 12 zote zikiwa zimetengenezwa na kampuni maarufu ya Leica, kamera ya mbele au (selfie camera) inayo Megapixel 8 yenye uwezo wa kuchukua picha zenye resolution ya 1080p, kuhusu battery simu hii inatumia battery yenye 4,000mAh yenye uwezo wa kukaa na chaji siku mbili (kutokana na matumizi yako).
Simu hii inategemewa kutoka kwanza kwa nchi za China, Europe pamoja na marekani kabla ya kufika nchi zingine. Kuhusu bei simu hii imetangazwa kwa bei ya Euro tu ambayo itauzwa kwa euro €699 ambazo ni sawa na shilingi za tanzania Tsh 1,700,000.
Je unasemaje kuhusu simu hii..? unaweza kutuandikia maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.