Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Huawei Yaja na Simu Mpya ya Huawei Y6 2017

Huawei yazindua kwa siri simu mpya ya Huawei Y6 ya mwaka 2017
Huawei-Y6-2017 Huawei-Y6-2017

Siku za karibuni kampuni ya huawei imezindua simu mpya ya Huawei Y6 ya mwaka 2017, wote tunajua toleo la mwaka 2015 lakini simu hii ya sasa ni tofauti kidogo na toleo la miaka miwili iliyopita.

Simu hii kwa sasa inaonekana kwenye website maarufu ya huawei ya ufaransa na bado hukuna habari zaidi kuhusu bei na simu hiyo itanza kutoka inchi gani kwanza, kutokana na tangazo hilo kwenye tovuti hiyo simu hiyo inaonekana kuwa na sifa zifuatazo. 

Advertisement

Kwa upande wa kioo simu hiyo inaonekana kuwa na kioo chenye inch 5 huku kikiwa na teknolojia ya HD IPS display pamoja na resolution ya 720×1280 pixel, kwa upande wa processor simu hiyo ya huawei y6 2017 inatumia  processor ya octa-core MediaTek MT6737T yenye uwezo wa 1.4 GHz ambao unasaidiwa na RAM ya GB 2. Vile vile simu hiyo ina ukubwa wa memory ya ndani ya GB16 ukubwa unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card mpaka ya GB 128.

Kwa upande wa mfumo simu hii inatumia mfumo wa Android toleo la 6 (Android Nougat) uku ikiboreshwa na mfumo wa Huawei wa EMUI 4.1, tukiamia kwenye kamera simu hii inayo kamera yenye uwezo wa megapixel 13 kwa kamera ya nyuma pamoja na kamera ya megapixel 2 kwa kamera ya mbele. Kwa upande wa chaji simu hii imewekewa battery kubwa ya 3000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa siku moja na zaidi kutokana na matumizi yako.

Kwa upande wa Network simu hii inauwezo wa 4G LTE, Wi-Fi (802.11b/g/n), Bluetooth 4.0, GPS/AGPS/Glonass, na kwa muunganisho simu hii ya huawei y6 2017 inatumia microUSB port, pamoja na sensor za Proximity sensor, Digital Compass, accelerometer pamoja na Ambient light sensor. Simu hiyo ina urefu wa 143.8 x 72 x 8.45mm pamoja na uzito wa  gramu 150.

Na hizo ndizo sifa ambazo ziliandikwa kwenye website hiyo ambapo simu hiyo ilionekana gafla bila kampuni ya huawei kufanya uzinduzi au kutoa taarifa yoyote kwenye vyombo vya habari. Kwa sasa hakuna habari zingine zenye kuelezea simu hiyo itaingia sokoni lini na kwa bei gani lakini inawezekana simu hiyo kuja hata Tanzania hivyo kaa karibu nasi kupata habari kamili kuhusu simu hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video. 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use