Hivi karibuni huko nchini Singapore kampuni ya Huawei imegawa power bank kwa wateja wa Apple waliokuwa kwenye mistari kusubiri kununua simu mpya za Apple.
Tukio hilo limetokea wiki iliyopita kwenye moja ya duka la Apple ambapo wateja walikuwa wamekesha wakisubiri duka hilo kufunguliwa asubuhi yake ili waweze kununua simu hizo za Apple kwa mara ya kwanza.
Inasemekana kuwa kwenye duka hilo lilikuwa na wateja wa Apple zaidi ya 200 ambao waligawiwa power bank hizo za kisasa ambazo zinasemekana kuwa na battery yenye uwezo wa 10,000 mAh ambayo inatosha kuchaji simu mbili zenye uwezo wa 4000mAh.
Kampuni ya Huawei ilikuwa ikitoa chaji hizo zilizokuwa na ujumbe, Here’s a power bank. You’ll need it. Courtesy of Huawei.” ikiwa na maana “Hii hapa ni power bank. Utahiitaji. Haki ya Huawei”. utani huu umekuja baada ya simu mpya za iPhone kuzinduliwa zikiwa na uwezo mdogo wa chaji na kushindwa na Huawei P20 ambayo yenyewe inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa 4000 mAh.
Pia hivi karibuni kampuni ya Huawei imeipita kampuni ya Apple na kuwa kampuni ya pili kwa uuzaji wa simu za mkononi maarufu kama smartphone.