Huawei, Vivo, Oppo na Xiaomi Kuja na Soko la Pamoja la Apps

Kampuni hizi zitawezesha wabunifu kuweka apps kwenye masoko mbalimbali
Huawei, Vivo, Oppo na Xiaomi Kuja na Soko la Pamoja la Apps Huawei, Vivo, Oppo na Xiaomi Kuja na Soko la Pamoja la Apps

Kampuni za Huawei, Vivo, Oppo na Xiaomi hivi karibuni zimetangaza kuungana kwa pamoja kwaajili ya kutengeneza soko jipya la pamoja la Apps ambalo litakiwa linasaidia wabunifu wa programu kuweka programu zao kwenye masoko yote ya kampuni hizi kupitia sehemu moja.

Kama unakumbuka, kampuni ya Huawei tayari inayo soko lake la programu ambalo linaitwa App Gallery, soko ambalo ni maalumu kwa watumiaji wa simu za Huawei. Pia ikumbukwe kuwa, soko la Play Store halipatikani kwa watumiaji wa simu za Android wa nchini China hivyo hatua hii itazidi kuongeza nguvu kwa kampuni hizo maarufu za nchini China.

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Reuters, umoja huo wa kampuni upo kwa lengo la kusaidia wabunifu kuweza kusambaza apps zao kwa urahisi na kufikia watu wengi zaidi ikiwa pamoja na uwezo wa kutengeneza pesa kutokana na Apps zao. Kwa sasa umoja huo umepewa jina la Global Developer Service Alliance au (GDSA) na kwa mujibu wa tovuti yake, utasaidia wabunifu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo nchi za India, Indonesia, Malaysia, Russia, Spain, Thailand, Philippines, pamoja na Vietnam.

Huawei, Vivo, Oppo na Xiaomi Kuja na Soko la Pamoja la Apps

Tokea kampuni ya Huawei ilipo letewa vikwanzo na marekani, kampuni hiyo imeonekana kutafuta njia mbalimbali za kuto kutegemea bidhaa kutoka nje ya China na hivyo sio kitu cha ajabu kuona kampuni ya Huawei ikiwa kwenye list ya kampuni zinazo unga mkono juhudi za kutengeneza soko la Pamoja kwaajili ya wabunifu kutoka nchi ambazo haziruhusiwi kutumia soko la Play Store.

Kwa sasa hata hapa kwetu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla bado hatuna sehemu moja ya kiafrika ya kuweka apps zetu, pengine huu ni wakati wa sisi kufikiria pia kuwa na sehemu ya kwetu wenyewe ya kuweka apps za kitanzania na kiafrika kwa ujumla..

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use