Huawei Yazindua Laptop Mpya ya Huawei MateBook 13

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya laptop mpya ya Huawei MateBook 13
Huawei Yazindua Laptop Mpya ya Huawei MateBook 13 Huawei Yazindua Laptop Mpya ya Huawei MateBook 13

Bado tuko kwenye mkutano wa CES 2019 na muda mchache uliopita kampuni ya Huawei Imezindua laptop yake mpya ya Huawei MateBook 13. Laptop hii ni toleo jipya la laptop ya Huawei MateBook X Pro iliyozinduliwa rasmi mwaka jana 2018.

Huawei MateBook 13 inakuja na kava la Aluminium ambalo limezunguka laptop hiyo na kuifanya ionekane kama laptop ya MacBook Air lakini tofauti yake ni kuwa, MateBook 13 ni nyembamba zaidi huku ikiwa na mm14.9, tofauti na MacBook Air ambayo inasemekana kuwa na mm15.9. Mbali na hayo MateBook 13 inakuja ikiwa na kioo kikubwa ambacho kina kingo ndogo sana huku kioo kikiwa zaidi ya asilimia 88 ya laptop yote.

Advertisement

Huawei Matebook 13 CES 2019

Kioo cha laptop hii kinakuja na uwezo wa Touchscreen chenye resolution ya 2160 x 1440 pixel, pamoja na uwezo wa HD. MateBook 13 inaendeshwa na processor ya 8th-generation Intel Core i7-8565U chipset ambayo inasaidiwa RAM ya GB 8, MateBook 13 inatumia Graphics card ya NVIDIA GeForce MX150 ambayo inauwezo wa kuchaza game nzito kama kawaida.

Laptop hii inasemekana kudumu na chaji kwa msaa 10 kama unaangalia video za 1080p na inaweza kudumu zaidi kama unatumia kwa matumizi ya kawaida. Kwa upande wa viunganishi MateBook 13 inakuja na USB C ports, lakini pia unapewa waya wenye uwezo wa kutumia USB A, USB C, VGA na HDMI.

Laptop hii pia inakuja na matoleo mengine yenye utofauti kwenye processor lakini laptop zote zinakaribia kufanana kwa sifa nyingine za ndani. Kwa upande wa bei ya Matebook 13, laptop hii inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni ikiwa inauzwa dollar za marekani $1000 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 2,300,000 bila kodi.

Kwa sasa hayo ndio machache ambayo tunajua kuhusu laptop mpya Huawei MateBook 13. Kwa sasa endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza mengine mengi kuhusu teknolojia zote mpya zitakazo zinduliwa kuanzia kesho kwenye mkutano wa CES 2019 hivyo hakikisha unakaa karibu nasi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use