Kampuni ya china maarufu kama Huawei hivi karibuni imeanza kutuma mialiko kwaajili ya mkutano wake wa uzinduzi wa simu yake mpya hapo November 3, habari za tetesi zinasema kuwa huawei wanategemea kuzindua simu yao mpya aina ya Huawei Mate 9 kwenye mkutano huo ambao utafanyika huko Munich Ujerumani.
Mkutano huo utaongozwa na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo ya Huawei Mr Richard Yu, ambaye yeye mwenyewe ataitambulisha simu hiyo mpya ya Huawei Mate 9. Habari kutoka tovuti ya Android Authority zinasema kutokana na Mr Richard mwenyewe kuwepo kwenye mkutano huo hii ni dalili ya kuwa kuna jambo kubwa kutoka kwenye kampuni hiyo maarufu ya utengenezaji wa simu za bei nafuu.
Hata hivyo hivi karibuni kiongozi huyo alizindua simu mbili aina ya Nova pamoja na Nova Plus ambazo zote zilizinduliwa kwenye mkutano wa IFA uliofanyika hivi karibuni, Simu hizo zote mbili zinaendeshwa na processor ya Qualcomm’s Snapdragon 625 pamoja na RAM ya GB 3 zikiwa na memory ya ndani ya GB 32 na uwezo wa battery wa mAh 3,020 kwa Huawei Nova na mAh 3,340 kwa Nova Plus, uwezo ambao utaziwezesha simu hizo kudumu na chaji kwa siku mbili mfululizo ukiwa unafanya matumizi ya kawaida (Huawei ilitangaza).
Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali Huawei watazindua simu yao hiyo mpya ya Mate 9 ambayo inategemewa kuwa na sifa kubwa kama vile processor mpya ya Kirin 960 pamoja na RAM ya GB 6 ikiwa na Memory ya ndani kuanzia GB 256, kamera mbili za nyuma kutoka kampuni ya Leica, vyote vikiwa vinaendeshwa na battery yenye uwezo wa mAh 4,000.
Je unataka kujua zaidi kuhusu simu hiyo mpya ya Mate 9 pamoja na kuangalia Live mkutano wa uzinduzi wa simu hiyo hapo November 3 ? basi endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.