Kampuni yenye makao yake makuu huko china Huawei imetangaza rasmi hapo jana kuwa siku ya leo tarehe 7 kampuni hiyo itazindua simu yake mpya ambayo itakuwa na jina la brand ya Honor Concept.
Simu hiyo ambayo inategemewa kutoka leo inategemewa kuja kwa aina tofauti kwani kwa mujibu wa tovuti ya GizmoChina ya china inadai kuwa simu hiyo haitakuwa na sifa za simu ya kawaida ikiwa haina camera wala speaker, badala yake vitu hivyo vitauzwa kama ziada.
Tetesi zingine kutoka mtandaoni zinasema kuwa simu hiyo itakuja na kioo kilichojikunja (curved display) kutoka samsung, vilevile tetesi hizo zinadai kuwa simu hiyo itakuja na teknolojia ya huawei ya (Huawei’s fast charging battery technology) ambayo itawezesha simu hiyo kujaa chaji asilimia 50 kwa dakika chache tu zakuchaji simu hiyo.
Simu hiyo inauwezekano wa kuuzwa nchini china pakee na kwa uchache sana, ili kupata habari kamili za simu hiyo na itauzwa kwa nchi zipi..? endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku na pia unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.