Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tetesi : Huawei Kuzindua Mfumo Mpya wa Hongmeng OS Wiki Hii

Huwenda hivi karibuni ukashuhudia muonekano wa mfumo wa Hongmeng OS
Tetesi : Huawei Kuzindua Mfumo Mpya wa Hongmeng OS Wiki Hii Tetesi : Huawei Kuzindua Mfumo Mpya wa Hongmeng OS Wiki Hii

Najua umesikia mengi sana kuhusu mfumo wa Hongmeng OS kutoka kampuni ya Huawei, mfumo ambao awali ulikuwa unatambulika kama mfumo ambao utakuwa mbadala wa mfumo wa Android baada ya kampuni ya Huawei kuzuiwa kwa muda kutumia mfumo wa Android kwenye simu zake mpya.

Hata hivyo, siku chache baada ya kampuni ya Huawei kuruhusiwa kuendelea kufanya biashara na kampuni za Marekani, kampuni hiyo ilitangaza kuwa mfumo wa Hongmeng OS sio mbadala wa mfumo wa Android bali ni mfumo ambao umetengezwa kwa ajili ya vifaa vingine mbalimbali kutoka kampuni hiyo.

Advertisement

Sasa hivi leo habari mpya kutoka tovuti ya Globaltimes ya nchini China, inasemekana kuwa kampuni ya Huawei ipo mbioni kuzindua mfumo wake huo wa Hongmeng OS ndani ya robo ya mwisho ya mwaka huu 2019, ripoti hizo zinadai kuwa inawezekana kuwa mfumo huo ukazindulkiwa ndani ya kipindi cha siku chachezijazo au wiki moja inayofuata.

Mbali na hayo, tovuti hiyo imeandika kuwa, mfumo huo utakuja ukiwa unatumika kwenye simu za bei nafuu za Huawei huku ikisemekana simu hizo zinategemewa kuanzia yuan 2,000 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania Tsh 654,000.

Hata hivyo inasemekana kuwa mfumo huo utazindui kwenye mkutano wa wabunifu wa Huawei ambao unategemea kufanyika tarehe 9 August huko Dongguan, nchini China. Kupata taarifa zaidi kama mfumo huo utazinduliwa siku hiyo endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use