Baada ya mgogoro wa kibiashara na serikali ya marekani, kampuni ya Huawei hivi karibuni ilitangaziwa kurusiwa tena kuanza kufanya biashara na kampuni za marekani. Maamuzi hayo yalifanywa na raisi wa marekani Donald Trump kupitia mkutano wa G20 uliofanyika mwezi uliopita.
Hata hivyo habari mpya kutoka tovuti ya Reuters zinadai kuwa, kampuni za marekani zinategemewa kuanza kupewa kibali maalum cha kuanza kufanya biashara na kampuni ya Huawei ndani ya wiki mbili au mwezi mmoja ujao.
Hata hivyo vibali hivyo vinategemewa kutolewa kwa kampuni ambazo zinapendelea kufanya biashara na kampuni ya Huawei ambayo hadi sasa bado ipo kwenye list ya kampuni zinazopingwa kufanya biashara na Marekani. Vile vile inasemekana kuwa moja kati ya kampuni ambazo zinategemewa kuchukua kibali hicho ni kampuni ya Google ambayo ndio ina miliki mfumo wa Android.
Google ilisitisha vibali vyake kwa kampuni ya Huawei kutumia mfumo wa Android miezi miwili iliyopita ikiwa ni hatua ya kutii sheria iliyowekwa na raisi wa marekani Donald Trump ambayo inazitaka kampuni zote za marekani kusitisha kufanya biashara na kampuni ya Huawei.
Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili kama Huawei itaendelea kutumia mfumo wa Android au itaendelea na harakati za kusajili mfumo wake ambao unasemekana sasa kusajiliwa kwa jina la Harmony huko chini za umoja wa ulaya.
Kujua habari zaidi kuhusu hili hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech na tutakujuza habari zote kuhusu teknolojia ikiwa pamoja na hili.