Kampuni ya simu Infinix inamatoleo mbalimbali ya simu ambapo toleo kubwa ni Infinix ZERO series, ikifuatiwa na Infinix NOTE Series, kisha HOT series na mwisho ni Smart Series. Infinix imeorodhesha matoleo yake kwa mfumo huu ili kuhakikisha kila mwenye uhitaji wa smartphone aweze kumiliki.
ZERO ULTRA
Mnamo October Mwaka huu kupita series ya ZERO, Infinix ilizindua rasmi Infinix ZERO ULTRA 5G ambayo inaifanya kampuni ya simu Infinix kushikilia nafasi ya kwanza duniani kuwa na simu yenye fast charge ya watt 180 ambayo ndio simu ya kwanza duniani kujaza chaji asilimia 100 ndani ya dakika 12 kutokea asilimia 0.
Infinix ZERO pia inafahamika kama simu ya kwanza duniani kuwa na camera ya Megapixel 200+OIS nyuma. Baada ya kuthibutishwa na wataalam wa Anga @royalmuseumsgreenwich imethibitika Infinix ZERO ULTRA ni simu yenye uwezo wa kuchukua picha za anga na kuchukua picha za matukio ya mtikisiko pasipo kuwa na ukungu.
NOTE 12 VIP
Series ya NOTE inatambulika na Kampuni hii kuwa series ya watu wasio na makeke ila ufanisi katika kazi ndio wanachozingatia na wengependelea simu ambayo inauwezo mkubwa wa kuchakata kazi kwa haraka. Infinix NOTE 12 VIP inatumia kichakata kazi kitaalamu CPU cha MediaTek G96 si rahisi kupata moto na inauwezo mkubwa wa kuendesha programs kubwa kwa haraka.
Kama inavyofahamika ni simu kwajili ya kazi, Infinix NOTE 12 VIP ina kioo mahiri aina ya AMOLED chenye utajiri wa rangi billion moja(1B) hivyo hutoa rangi halisi ya tukio la picha, video kulingana na rangi halisi ya eneo husika.
HOT 12
Toleo jengine ambalo hawa mabingwa wamelipa hadhi kubwa baada ya kupotea tolea la ‘S’ ni Infinix ‘HOT’ mabadiliko yameanza kuonekana kwenye HOT 12. Infinix HOT 12 pamoja ya kuwa ni simu yenye gharama nafuu kuzidi series ya NOTE lakini inafeatures mahiri, tukianzia na memory Infinix HOT 12 inakimbizana na series ya NOTE 12 zikiwa na GB128 ya ROM.
Infinix HOT 12 ni kimbilio la watu wenye kutumia muda mwingi wakiwa katika pirika pirika kama wasafiri n ahata wanaoishi maeneo yenye shida ya umeme. Infinix HOT 12 inabattery ya mAh 5000 yenye kudumu na chaji masaa 48 kwa matumizi ya kawaida.
SMART 6
Infinix Smart 6 ni simu pekee katika soko la simu kwa sasa yenye kigezo hiki kwa mujibu wa kampuni ya Infinix, umbo la nje la simu hii limetengenezwa na material maalumu lenye kuzuia virusi vya corona kuishi kwenye simu hiyo na kutua kwa mtumiaji. Sifa nyengine ni GB 64 ya Rom, Camera Megapixel 8, kioo inch 6.6 na battery mAh 5000.
UPATIKANAJI
Simu hizi zinapatikana kwa bei ya punguzo katika msimu huu wa sikukuu za Chrismas na Mwaka Mpya vile vile kupitia promosheni ya PIGA UTOBOE ukinunua kati ya simu hizo utajiweka katika nafasi ya kujishindia Pikipiki, Fridge na TV ya inch 65 tembelea maduka yote ya simu nchini usipitwe na ofa hizi.
Kwa huduma ya haraka piga 0712602970.