Jinsi kampuni ya Nokia ilivyo maliza mwaka uliopita kwa kutoa simu yake ya kwanza ya Android ya Nokia 6 (2017), hivi leo kampuni hiyo imerudi tana na maboresho ya toleo la simu hiyo ya Nokia 6 (2018) ambayo inakuja na maboresho mbalimbali ya muonekano pamoja na sifa.
Sifa za Nokia 6 (2018)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, 16M colors
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1.1 (Nougat), Updated kwenda Android 8.0 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53
- Uwezo RAM – GB 4
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 au GB 64 yenye uwezo wa kuongezeka kwa memory card hadi ya GB 256.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye uwezo wa (f/2.0, 1.12 µm), autofocus, na kuchukua picha na video za 1080 pixel.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/2.0, 1.0 µm), phase detection autofocus pamoja na dual-LED dual-tone flash, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
- Uwezo wa Network – 2G, 3G pamoja na 4G yenye 4G VoLTE,
- Uwezo wa Wifi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n huku ikiwa na teknolojia za Wi-Fi Direct na hotspot
- Uwezo wa Bluetooth – 5.0, A2DP, LE
- Uwezo wa GPS – A-GPS, GLONASS, BDS
- Uwezo wa USB – Type-C 1.0 reversible connector
- Uwezo wa FM Radio – Simu hii pia ina fm radio yenye uwezo wa RDS
- Uwezo wa Fingerprint – Inayo Fingerprint iliyoko kwa nyuma
- Aina za Sensor – Simu hii ina sensor za accelerometer, gyro, proximity pamoja na compass
- Uwezo wa Battery – Simu hii ina uwezo wa battery isiyotoka ya Li-Ion yenye uwezo wa 3000 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji siku nzima.
- Bei – Simu hii inauzwa kwa Euro €220 sawa na dollar za marekani $265.04 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 600,000 kwa mujibu wa viwango vya fedha vya siku ya leo.
- Rangi – Nokia 6 (2018) inakuja na rangi za Nyeusi na Silver
Na hizo ndio sifa kamili za simu mpya ya Nokia 6 (2018) kutoka kampuni ya Nokia ambayo sasa inasimamiwa na kampuni ya HMD Global kutoa simu zake mbalimbali. Je unaonaje sifa za simu hii..? tuambie kwenye maoni hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.