Ni wazi kuwa mfumo wa akili bandia au Artificial Intelligence (AI) sasa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, uwe wewe ni mwana teknolojia au lah AI sasa ni sehemu muhimu ya kazi, michezo au baadhi ya huduma ambazo unatumia kila siku.
Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakuonyesha aina mbalimbali za browser ambazo zimeunganishwa na mifumo mbalimbali ya akili bandia na kufanya browser hizo kuwa rahisi kutumia na pengine bora kuliko browser nyingine. Basi moja kwa moja twende kwenye makala hii.
Microsoft Edge Copilot AI
Microsoft Edge ni browser ambayo ina tengenezwa na microsoft ambayo sasa ni sehemu ya kampuni ya Open AI ambayo ndio kampuni kiongozi kwenye ubunifu na utengenezaji wa teknolojia za AI, hii ni kupitia mfumo wa ChatGPT.
Sasa browser hii ambayo inapatikana kwenye mfumo wa Windows, pamoja na Android inakupa uwezo wa kutumia Copilot AI kufanya mambo mbalimbali.
Download Microsoft Edge Copilot
Brave Leo AI
Brave ni aina nyingine ya Browser ambayo ni maarufu na inatumiwa na watu wengi sana, mbali ya kuwa maarufu sasa browser hii inakuja na uwezo wa AI ambao utakusaidia kufanya mambo mbalimbali. Kama ilivyo Microsoft Edge, hii nayo ni sehemu ya browser inayotumia mfumo kama wa Google Chrome.
Mfumo wa Leo AI utakusaidia kufanya mambo mbalimbali kama kutoa muhtasari wa makala mbalimbali, kutoa majibu ya maswali mbalimbali na mengine mengi. Leo AI inatumia mfumo wa ChatGPT na inafanya kazi sawa na Microsoft Edge Copilot AI.
Opera Aria Browser AI
Opera Mini au Opera ni browser maarufu sana hasa kutokana na kuwa na sifa mbalimbali ambazo ni rahisi kwa watumiaji wengi. Pia Opera ni moja ya browser inayotumiwa sana na watanzania wengi kutokana na uwezo wake wa kudownload.
Sasa kupitia browser hii sasa utaweza kutumia mfumo wa AI kupitia Opera Aria Browser AI, pia utaweza kufanya mambo mbalimbali kama vile kutoa muhtasari wa makala, kujibu maswali mbalimbali kwa kutumia mfumo wa chat.
Download Opera Aria Browser AI
Arc Max
Arc Max ni browser mpya ambayo inakuja kwa kasi sana na inauwezo wa kutumia mfumo wa AI kufanya mambo mbalimbali. Kwa sasa browser hii inapatikana bila AI kupitia soko la App Store huku mfumo wa Windows ukiwa unatrajiwa kuja hivi karibuni.
Voilà
Browser nyingine mpya ambayo unatakiwa kutumia kama unataka kutumia mfumo wa AI ni pamoja na browser ya Voilà browser hii ni nzuri sana utaweza kutumia mfumo wa ChatGPT 4 moja kwa moja kupitia ndani ya browser hii.
Mbali na hayo utaweza kutengeneza makala mbalimbali kwa kuchat na sehemu ya AI ndani ya browser hii. Unaweza kujaribu browser hii kupitia mfumo wa Available for Chrome, Edge, Firefox na Safari.
Na hizo ndio baadhi ya browser zenye kuweza kutumia mfumo wa AI kuweza kurahisha matumizi yako ya kila siku. Kama unataka kujifunza zaidi kupitia Tanzania Tech hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech kupitia kwenye simu yako. Kumbuka kubadilisha Lugha kuwa kiswahili kusoma makala hizi.