HABARI ZA HIVI PUNDE zinasema kuwa kuna mtu ameingia kwenye makao makuu ya mtandao wa YouTube akiwa na silaha na inasemekana watu kadhaa wame jeruhiwa na wengine tayari wamesha waishwa Hospital.
Kwa mujibu wa ripoti za muda huu kutoka mtandao wa The Verge, Polisi wa kitongoji cha San Bruno nchini marekani ambapo ndipo makao hayo makuu yalipo wamefika kwenye eneo la tukio na kuwatoa nje wafanyakazi wa mtandao wa Youtube zaidi ya 1500 huku wakiwa wameweka mikono kichwani.
Bado haija julikana chanzo cha mtu huyo kuingia ndani ya makao hayo makuu na vilevile pia bado haijajulika idadi ya watu walio jeruhiwa ikiwa pamoja na mtuhumiwa huyo. Tutawaletea habari kamili hapo kesho.. endelea kutembelea Tanzania Tech.
Updated 4/4/2018 – Mwenyekiti Mtendaji wa Google Sundar Pichai Ameandika Barua Kuhusu Tukio Hili.
Katika muendelezo wa taarifa kuhusu mtu kuingia na bunduki kwenye makao makuu ya YouTube, mwenye kiti mtendaji wa kampuni ya Google ametoa waraka kuhusu tukio hilo huku akiwapa pole wafanyakazi wanne walio jeruhiwa kwenye tukio hilo lililo tokea hapo jana saa tano usiku kwa saa za afrika mashariki.
Kwa sasa kama ilivyo thibitishwa kwenye barua ya mwenyekiti huyo ni watu wanne tu ndio walio jeruhiwa kwenye tukio hilo na ni salama kusema kuwa hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha.
Here is the note that @sundarpichai just sent to Googlers worldwide. pic.twitter.com/bdC6KeTl9c
— Google Communications (@Google_Comms) April 3, 2018
Updated – 4/4/2018 Saa 9:11AM – Imethibitishwa Mtu Aliyeingia na Silaha makao makuu ya YouTube Amejiua
Kwenye muendelezo wa Habari hii habari kutoka kwenye mtandao wa BBC zinasema kuwa mwanamke wa miaka 39 anaye julikana kwa majina ya “Nasim Najafi Aghdam” ndie aliyeingia kwenye makao hayo makuu ya YouTube akiwa na silaha na kujeruhi wafanyakazi wanne wa mtandao wa YouTube. Aidha ripoti zinasema kuwa mwanamke huyo baada ya kufanya tukio hilo ali jiua kwa kujipiga risasa akiwa ndani ya jengo la makao makuu ya mtandao wa YouTube.
Thanks for the update bigup sanaaaaa