Kampuni ya maarufu ya utengenezaji wa simu ya HTC hivi karibuni inategemewa kuzindua simu yake mpya ambayo inaitwa HTC Bolt, Habari za tetesi kutoka tovuti mbalimbali zinasema simu hiyo ambayo inafanana kwa muonekano na simu kutoka kampuni hiyo yaani HTC 10 inategemewa kutoka kuanzia tarehe 18 mwezi huu.
Habari hizo zinaendelea kusema kuwa simu hiyo kutoka kampuni hiyo ya Taiwan inategemea kuja bila sehemu ya kuweka earphone maarufu kama (Earphone jack) vilevile tetesi hizo zinaelekeza kuwa simu hiyo inasemekana kuwa itakuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android 7.0 Nougat. Kuhusu sifa zingine za simu hiyo mpya ya HTC Bolit ni pamoja na kioo cha 5.5-inch pamoja na memory ya ndani kuanzia 64GB ikiwa inaendeshwa na RAM ya GB 3, kwa upande wa kamera simu hiyo inategemewa kuja na kamera ya mbele yenye uwezo wa 18-megapixel.
Kuhusu bei ya simu hiyo bado haijajulikana ila inawezekana kuuzwa bei nafuu kuliko simu ya mwaka huu kutoka kapuni hiyo yaani HTC 10. ili kujua sifa kamili za simu hiyo na pale itakapo toka endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.