Serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo siku ya tarehe ilimetoa amri ya kufungwa kwa mitandao yote ya kijamii ili kuzuia usambazaji wa picha na video za ghasia zinazoendelea.
Aidha hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la upinzani dhidi ya rais Joseph Kabila ambaye amekataa kujiondoa madarakani wakati awamu yake inamalizika mwezi Desemba hata hivyo Migomo ya kitaifa ilipangwa kufanyika siku za Jumanne na Jumatano iliyopita.
Mapigano ya Jumatatu baina ya kundi la Bundu dia Kongo na vikosi vya usalama ,yalipelekea vifo vya watu 14 na wakati wengine wengi wakijeruhiwa vibaya.
Mkuu wa idara ya mawasiliano nchini humo Oscar Manikunda Musata amefahamisha kwamba mitandao ya kijamii kama Twitter, WhatsApp ,Facebook na Instagram itafungwa kwa muda mpaka hapo itakapo tangazwa tena.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : Amnesty International