Ikiwa kama vile leo ni siku ya kompyuta hapa Tanzania Tech, hatimaye kampuni ya microsoft yafanikiwa kuzindua laptop yake mpya ya Surface. Laptop hii imezinduliwa kwenye mkutano wa Microsoft EDU ulio fanyika leo huko New York nchini marekani.
Laptop hii ina kioo cha inch 13.5 ikiwa na teknolojia ya PixelSense display, kwa upande wa processor laptop hii inakuja na processor za Intel Core i5 na i7 processors zikiwa na uwezo wa hard disk mpka terabit 1 pamoja na RAM ya 4GB. Vilevile laptop hii ina uwezo wa kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 14 pale inapochajiwa vizuri hivyo kukupa muda wa kutosha kufanya shughuli zako za kila siku, Laptop hii pia imetengenezwa maalum kwa ajili ya wanafunzi kwani inakuja na toleo jipya la Windows 10 S toleo ambalo sasa linapatikana kwaajili ya wanafunzi na walimu wote kote duniani.
Laptop hii ambayo inategemewa kutoka mwezi huu tarehe 14 inategemewa kuuzwa kwa dollar za kimarekani $999 sawa na shilingi za kitanzania 2,300,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo tarehe 2 may 2017.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
Naweza kupataje hii laptop
Itabidi utafute mtandaoni