Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Haya Ndio Mambo 6 Uliyokuwa Hujui Kuhusu Teknolojia

Haya ndio mambo ambayo nahisi ulikua huyajui kuhusu teknolojia
Haya Ndio Mambo 6 Uliyokuwa Hujui Kuhusu Teknolojia Haya Ndio Mambo 6 Uliyokuwa Hujui Kuhusu Teknolojia

Ni jumapili tena na kama tunavyojua Teknolojia imekua sana ukilinganisha na miaka ya nyuma, mambo mengi sana yamebadilika na mengine yakibaki kwenye historia na kuweza kutengeneza list hii ya mambo 6 ambayo ulikuwa huyajui kuhusu teknolojia.

6. Logo ya Kwanza ya Apple

Advertisement

Apple ni kampuni ambayo imeanza kitambo kidogo, kama zilivyo kampuni nyingine Apple imekua ikibadilika kadri siku zinavyo kwenda. Mwaka 1977 mchoraji Rob Janoff alibuni logo ya kwanza a Apple na ilikuwa ina picha ya Isaac Newton akiwa amekaa chini ya mti.

5. Internet Ina Siku 10486 toka Kuanzishwa

Kwa wale ambao ni wageni kwenye hili ni kuwa, ugunduzi wa internet ulianza miaka ya 1950 hadi kufikia mwaka ya 1960, wizara ya ulinzi ya marekani ilifanikiwa kutengeneza mfumo ulio-itwa ARPANET na hadi tarehe 1 January 1983 mfumo huo ulibadilishwa na kuweka kwenye mfumo wa TCP/IP na kuanzia hapo wagunduzi mbalimbali walianza kuunganisha kompyuta moja na nyingine na hatimaye mwaka 1990 mgunduzi wa kompyuta Tim Berners-Lee ali anzisha mfumo wa (www) au World Wide Web ambao sasa ndio unatumiaka kuunganisaha tovuti mbalimbali duniani.

4. Hard Disk Kubwa Kuliko Zote Duniani

Linapokuja swala la ukubwa wa kuifadhi data ukweli ni kwamba kila kitu cha kidigitali siku hizi kinategemea uwezo wa kuhifadhi lakini je ulishwa wahi kujiuliza ukubwa wa kuhifadhi mwisho wake ni wapi..? Hapa ndipo tunapokuja kwenye list hii, hard disk kubwa kuliko zote duniani kwa sasa ina ukubwa wa TB 60 au terabyte 60, wote tunajua TB 1 ni sawa na GB 1000 sasa hard disk hii ina GB 60,000. Hard disk hii imetengenezwa na kampuni ya Seagate kutokana na ukubwa wake bado haijatangazwa rasmi bei yake…

3. Ugonjwa wa Kuhisi Simu Inaita

Mwanzo tulisha ongelea kuhusu dalili za ugonjwa wa kupenda smartphone, lakini leo hapa nataka nikujulishe kuwa Phantom Vibration Syndrome huu ni ugonjwa au ni jina linalotumiwa na madaktari kumuita mtu mwenye tatizo la kuhisi simu ina toa mlio wa kuita au ku-vibrate.

2. Huyu Ndie Anaelipwa Pesa Nyingi Youtube

Kwa sasa PewDiePie ndio jina la channel ya Felix Arvid Ulf Kjellberg ambaye yeye ndio anaongoza kwa kulipwa pesa nyingi zaidi na mtandao wa YouTube. Analipwa karibia dollar za marekani Milioni 15 kwa mwaka sawa na karibia shilingi za kitanzania Tsh 33,808,500,00.

1. Watu 3 tu Duniani Ndio Wanaojua Viungo vya Kutengeneza Cocacola

Hii ndio sehemu ambayo kampuni ya Cocacola inahifadhi viungo vya soda yake ya cocacola, inasemekana kuwa watu wa tatu tu! duniani ndio wanao jua viungo hivyo na wao ndio wanao ruhusiwa kuingia ndani ya sehemu hii.

Na hayo ndio mambo sita ambayo nimekuletea jumapili ya leo, kujifunza mengine mengi kuhusu historia ya teknolojia ungana nasi kila jumapili kwenye kipengele cha Je Wajua. Pia unaweza kujiunga na mitandao yetu ya kijamii kuweza kuwa wa kwanza kujua yote kuhusu teknolojia.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use